logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sijakufa!Msanii Mwana Mtule atupilia mbali madai kuwa ameaga dunia

Bado niko hai πŸ™πŸ™πŸ«‚...Polisi bado wanaendelea na uchunguzi Kwa washukiwa πŸ™πŸ«‚πŸ«‚."

image
na Radio Jambo

Makala28 October 2023 - 05:46

Muhtasari


  • Mtule amesema kwamba polisi wanaendelea kuchunguza kisa hicho ili kuwakamata waliohusika.

Msanii wa nyimbo za injili Nchini Mwana mtule kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram amekanusha na kutupilia mbali madai kwamba ameaga dunia.

Hii ni baada ya kuripotiwa kuwa msanii huyo ameaga dunia.

Hata hivyo ameweka wazi kwamba alipewa sumu alipokuwa kwa rafiki yake eneo la Rongai.

Mtule amesema kwamba polisi wanaendelea kuchunguza kisa hicho ili kuwakamata waliohusika.

"Habari Familia πŸ™πŸ˜ž Haya sio kutafuta kiki tafadhali acheni kuniandikia R.I.P

Sijafa, namshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yangu Nililishwa sumu Mahali pa Marafiki, eneo la RONGAI."

Aliongeza;

"Nitazungumza nanyi hivi punde niwaeleze kilichotokea maana Sasa bado sijisikii vizuri πŸ™πŸ™ Mungu awabariki wote

Bado niko hai πŸ™πŸ™πŸ«‚...Polisi bado wanaendelea na uchunguzi Kwa washukiwa πŸ™πŸ«‚πŸ«‚."

Wasanii wengi Nchini wanafahamika kwa kutafuta kiki kutoka kwa mashabiki ili kusukumavibao vyao ilhali Mtule amekana na kusema kwamba sio kiki anatafuta.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved