Staa wa muziki wa Bongo Diamond Platnumz amemeuomba anayekesiwa kuwa mpenzi wake ambaye pia ni msanii wa WCB, Zuhura Othman almaarufu Zuchu amzalie mtoto.
Diamond alifanya ombi hilo wakati walipokuwa wakitumbuiza jukwaani kwenye Tamasha za Wasafi Festival zililizoadaliwa kwenye uwanja wa Kahama, nchini Tanzania .
Bosi huyo wa WCB alimuacha huyo wake na mshangao mkubwa baada ya kumuibia maneno yaliyomguza roho akimnenea amzalie mtoto.
Wakati wakiimba wimbo 'Mtasubiri sana' Diamond aliimba "unanipenda me ....... unaniamini .... ...na "utanizalia? ",
Baada ya kuimba hivyo, wawili hao walikubatiana na kubusu, jambo ambaplo lilishabikiwa sana na wafuasi wao
Mastaa hao wawili wa muziki wa Bongo walikuwa pamoja wakicheza muziki kwenye Tamasha hizi ambazo zilijawa na bwebwe baada ya wafuasi wa Zuchu kufuraishwa na maneno ya msanii Diamond akimtaka amzalie.
Haya yanajiri siku chache baada ya msanii wa nyimbo za Taarab Khadija Kopa ambaye ndiye Mamake Msanii Zuchu kwenye mahojiano ya moja kwa moja kuweka wazi kuwa hafahamu mahusiano kati ya Bintiye na Diamond.
Kwa muda mrefu, Zuchu na Diamond wamedaiwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.