Rema avunja kimya kwa machozi ya furaha baada ya kutumbuiza hafla ya Ballon d'Or

Rema ndiye aliyekuwa msanii nguli kutoka Afrika kutumbuiza kwenye hafla hiyo ya soka na kuingia kwenye orodha fupi ya masupastaa wa Afrika ambao wamewahi tumbuiza kwenye hafla za kispoti.

Muhtasari

• Lionel Messi wa Argentina aliibuka mshindi akifuatiwa na Erlin Haaland, Kylian Mbappe, Kevin De Bruyne, Rodri, Vinicius Junior, Julian Alvarez.

Rema
Rema
Image: Instagram

Mwimbaji nyota wa Afrobeats Divine Ikubor anayejulikana kama Rema amejitokeza kwenye mitandao ya kijamii kudhihirisha furaha yake baada ya kupata nafasi adimu ya kutumbuiza kwenye hafla ya kutolewa kwa tuzo ya Ballon d’Or ya 2023.

Rema kwa mara nyingine tena anaendelea kuweka Afrobeats katika kiwango cha kimataifa na kwa ugani huwafanya Wanigeria kujivunia anapoimba wimbo wake wa "Calm Down" katika tuzo ya soka.

Tuzo hiyo ilifanyika jana jioni Oktoba 30, 2023 kwenye ukumbi wa Theatre du Chatelet huko Paris, Ufaransa.

Lionel Messi wa Argentina aliibuka mshindi akifuatiwa na Erlin Haaland, Kylian Mbappe, Kevin De Bruyne, Rodri, Vinicius Junior, Julian Alvarez.

Victor Osimehen anaifanya Nigeria kujivunia alipoorodheshwa nambari 8 duniani akifuatiwa na Bernando Silva na Luka Modric katika nafasi ya 10.

Rema katika post yake ya Instagram baada ya kutumbuiza anawashukuru Waandaji wa tuzo hiyo kwa nafasi hiyo na pia alitoa shukrani kwa Mungu.

Aliandika; "Afrobeat katika Ballon d'Or, ninashukuru sana kwa nafasi hiyo. Utukufu kwa aliye juu kwa neema. 🤲🏾❤️.”

Rema ndiye aliyekuwa msanii nguli kutoka Afrika kutumbuiza kwenye hafla hiyo ya soka na kuingia kwenye orodha fupi ya masupastaa wa Afrika ambao wamewahi tumbuiza kwenye hafla za kispoti.