logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Matusi kwenye ndoa ni ishara ya wapenzi kuchokana- Wema Sepetu

"Matusi si sehemu ya ndoa, ila alifai kushudiwa wakati wowote kwenye ndoa kwani ina hatari zake, " Wema alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani01 November 2023 - 09:34

Muhtasari


  • •Wema alibainisha kuwa wapenzi wanaopenda hupeana heshima kwa kila jambo wanalojishugulisha nalo.
  • •"Matusi si sehemu ya ndoa, ila alifai kushudiwa wakati wowote kwenye ndoa kwani ina hatari zake, " Wema alisema.

Staa muigizaji wa filamu bongo Wema Sepetu ametoa kauli kwa wapenzi wanaopitia ndoa zenye  changamoto  akisema kuwa ndoa zote zenye matusi na masegenyo tele huwa zimefikia kikomo kwa wapenzi kuchokana.

Mlimbwende huyo alibainisha kuwa wapenzi wanaopenda hupeana heshima kwa kila jambo wanalojishugulisha nalo na hakuna yeyote anayeweza kuwa na sababu ya kumwelekezea lugha chafu mwenziye.

"Wakati  wachumba wanaaza kurushiana cheche  za maneno kwenye ndoa, furaha ya mapenzi huwa imedidimia, jambo linalo punguza heshima na kuzoa vurugu ambazo mwishowe husababisha talaka kwa ndoa nyingi," alisema Wema.

"Matusi si sehemu ya ndoa, ila alifai kushudiwa wakati wowote kwenye ndoa kwani ina hatari zake, wawili wakipendana wadumishe ahadi zao na furaha ya milele, kamwe mpenzi akupendaye hawezi kunenea mabaya," aliongeza.

Muigizaji Wema aliyasema haya wakati alipokuwa akiwashauri wanandoa kupita kituo kimoja cha redio cha Tanzania.

"Wapenzi kwenye Ndoa wanafaa kuvumilia na kuepuka lugha chafu, kwa kwani inasababisha msongo wa mawazo kwa anayehelekezewa lugha hiyo,wengi wa waathiriwa ni wanawake mara kwa mara wanapokubana na mambo haya wengi uvumilia tu," alisema.

Wema Sepetualiwapa ushauri wanandoa kuwa mfano mzuri kwa wao wenyewe wakizingatia kuepukana na lugha chafu ya matusi inayochangia wapenzi wengi kuchokana na kuadhirika kiafya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved