Mulamwah apongezwa baada ya kuonyesha maendeleo makubwa ya jumba lake la kifahari (+video)

Makumi ya watu wakiwemo watu mashuhuri na mastaa wenzake wamempongeza kwa mafanikio yake.

Muhtasari

•Mulamwah alichapisha video iliyomuonyesha akiwa amesimama juu ya jengo hilo la ghorofa mbili ambalo linaendelea kujengwa.

•“POLE POLE TU, unaweza. Mungu amekuwa mkuu, mtu asikwambie HUWEZI!!," Mulamwah alisema.

Mulamwah.
Mulamwah.
Image: Facebook

Siku ya Jumanne, mchekeshaji mashuhuri wa Kenya David Oyando almaarufu Kendrick Mulamwah alionyesha maendeleo makubwa ya ujenzi wa jumba lake kubwa katika eneo la Kitale, kaunti ya Trans-Nzoia.

Mtumbuizaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye pia ni muuguzi alichapisha video ambayo ilimuonyesha akiwa amesimama juu ya jengo hilo la ghorofa mbili ambalo linaendelea kujengwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kueleza jinsi anavyojivunia mafanikio yake.

Pia alitumia fursa hiyo kumshukuru Mungu na kuwatia moyo vijana wengine kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika lengo la kutimiza ndoto zao.

“POLE POLE TU, unaweza. Mungu amekuwa mkuu, mtu asikwambie HUWEZI!!, jiamini, amini ndoto zako, omba Mungu na ujitahidi, ipo siku utakaa na kusema NIMEFANYA,” Mulamwah alisema kwenye sehemu ya maelezo ya video hiyo.

Mchekeshaji huyo pia alidokeza kuwa atakuwa akishiriki vidokezo vya mafanikio na vijana nchini jinsi ya kuwekeza na kuweka akiba.

Makumi ya wanamitandao wakiwemo watu mashuhuri na mastaa wenzake walimiminika chini ya posti hiyo kumpongeza kwa mafanikio yake.

Tazama maoni ya baadhi ya wanamtandao;

@blessednjugush: 👏🏻👏🏻👏🏻👏🏻

@celestinendinda Well done!

@iam_marwa This is the new flex, building Africa.

@anitatsalwa  Am happy for you

@marya_okoth Eeeish, see God.

@gkserkal Omwami good job kaka, to many more buildings, inafaa nitafute drone nipige ile yangu.

@mboya_vincent Wakireverse pesa tunachukua tunaendelea na kujenga

@babushkakenya: Hardwork pays siku zote.