logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Milly Chebby ajibu tetesi za kutemwa na Jackie Matubia kwenye insta

Tetesi za uwezekano wa kuwa na chuki kati ya wawili hao zimeibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki wao.

image
na

Habari02 November 2023 - 05:43

Muhtasari


• Katika siku za hivi majuzi,wawili hao walionekana kutengana kutokana na mwingiliano wao kuonekana kufifia na kutokuwa pamoja kwenye hafla kama ilivyokuwa hapo awali.

• Milly anashauri kuwa awamu hii katika urafiki wao ilikuwa msimu mwingine tu maishani ambayo ni sawa na misukosuko kila mmoja hupitia.

Milly Chebby na Jackie Matubia

Milly Chebby na Jackie Matubia wamekuwa marafiki kwa muda mrefu hadi kufikia hatua ambayo walidai kuwa walikuwa mandugu.Urafiki wao ulistawi na walikuewepo kila wakati kwenye hafla za kila mmoja.

Safari yao ya urafiki na kuwa pamoja iliwavutia wengi. Mashabiki wao walifurahia maudhui waliyounda,picha walizopiga pamoja na msaada wao kwa kila mmoja.

Katika siku za hivi majuzi,wawili hao walionekana kutengana kutokana na mwingiliano wao kuonekana kufifia na kutokuwa pamoja kwenye hafla kama ilivyokuwa hapo awali.

Tetesi za uwezekano wa kuwa na chuki kati ya wawili hao zimeibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki wao.

Mwezi uliopita,marafiki hao wawili,waliibua mijadala mitandaoni baada ya Matubia kukosa kuudhuria harusi ya kitamaduni ya Milly Chebby.

Katika kujibu,Matubia alifichua kwamba hakuwa katika maelewano mazuri na wanandoa hao.Matubia alikosa  kuudhuria sherehe hizo kwa madai ya  kuwa ana moyo mbaya na kwamba hana mume.

Imefikia hatua ya wawili hao kuacha kushabikiana kwenye mitandao huku wakiacha kufuatiliana kwenye Insta,jambo ambalo kulingana na kisasi cha sasa linaashiria kukatisha mahusiano.

Hata hivyo,baada ya Matubia kuchukua hatua ya kuacha kumfuatilia Milly kwenye ukurasa wa Insta ,Milly alijitokeza kufafanua hali hiyo,akionyesha kuwa hakujua kuhusu hatua yeyote ya kuacha kufuatiliana kwenye kurasa za mitandao.

Milly aliwahakikishia mashabiki kuwa angedhibitisha mara moja ikiwa Jackie ameacha kumfuatilia.

Milly anashauri kuwa awamu hii katika urafiki wao ilikuwa msimu mwingine tu maishani ambayo ni sawa na misukosuko kila mmoja hupitia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved