Baba levo ataka awekwe kwenye urithi wa Diamond Platnumz

Baba levo alisema Diamond ndiye babangu mlezi mwenye chuki aende mahakamani.

Muhtasari

• Baba levo anatajwa kuwa amemzidi umri msanii Diamond ila kulingana naye anamchukulia kama babake mzazi yuko tayari kumtumikia kama mwana.

Baba Levo na Diamond
Image: INSTAGRAM// BABA LEVO

Msanii wa Tanzania, Revokatus Kipando, almaarufu Baba Levo, amewashagaza wengi baada ya kufunguka wazi akisema kwamba anamchukulia Diamond kama Babake mzazi na anataka awekwe  kwenye urithi wa mali yake.

"Namchukulia Diamond kama babangu mzazi ananilea kama mwana, kwa maisha yangu vitu ninavyomiliki ni kutoka kwake nataka niwe mmoja wa wana watakaomiliki urithi wa Diamond,"alisema.

Msanii huyu pia aliweka picha kwenye ukurasa wa mtandao wake wa instragram picha ambayo amehariri akiwa na msanii Diamond picha ambapo ameweka maelezo..KWENYE URITHI   NIMOO ....BABA NA BABU.

Kwenye mahojiana ya moja kwa moja msanii huyu aliongeza kuwa yeyote anayekerwa na jambo hilo aelekee mahakamani kumshtaki kwani Diamond ndio mzazi anayemsaidia kwa maisha yake.

Baba levo anatajwa kuwa amemuzidi msanii Diamond Umri ila kulingana naye anamchukulia kama babake mzazi yuko tayari kumtumikia kama mwana.

"Kumzidi Diamond umri si jambo kubwa kwangu mimi naamini yeyote anayekushinda kifedha ni mkubwa kukuliko kwa hivyo Diamond ni mkubwa wangu nami ni mwana kwake namchukulia kama babangu",alisema Baba levo