"Bado niko single" Mulamwah akanusha kufunga harusi na rafiki yake Ruth K

Mimi kusettle ni mipango ya Mungu, kwa sasa hivi ni kutafuta pesa. Mimi nakuwa single muda wote, sina mpenzi,” alisema.

Muhtasari

• Mchekeshaji huyo pia aliwapiga mashabiki wake usinga wa uongo machoni akikataa kuzungumzia uvumi kwamba Ruth K ana mimba.

Mulamwah na mpenziwe
Mulamwah na mpenziwe
Image: Instagram

Mchekeshaji Mulawah amekanusha dai la kufunga harusi na rafiki wake wa karibu Ruth K wikendi iliyopita.

Katika mahojiano na waandishi wa habari za mitandanoni, Mulamwah alikanusha kwamba shughuli iliyuomuonesha wikendi akiwa na bestie wake Ruth K katika kile kilichoonekana kama harusi ya kitamaduni wala si harusi.

Alisisisitiza kwamba yeye bado yuko single na hana mpenzi akisema kwamba mambo ya Ruth K na mpenzi wake yeye hawezi ingilia.

“Kule kwa kina Bestie nilienda tu kutembea kwa vile pia yeye anajua kwetu lakini wali overreact, kufika nikapata maturubai ikabidi tu imekuwa sherehe lakini mimi sikutarajia,” alisema.

Mchekeshaji huyo pia aliwapiga mashabiki wake usinga wa uongo machoni akikataa kuzungumzia uvumi kwamba Ruth K ana mimba.

“Mimi sijui kama ako na mimba, hayo ni mambo yake na mpenzi wake, siwezi ingilia maisha yake, ni mwenyewe kuamua kufichua mimi siwezi zungumzia. Mimi kusettle ni mipango ya Mungu, kwa sasa hivi ni kutafuta pesa. Mimi nakuwa single muda wote, sina mpenzi,” alisema.