Bernice Saroni akanusha madai ya kumshawishi Edday Nderitu kubaki Marekani amlaumu Nyamu

Muhtasari

• Katika mahojiano na wanablogu, Saroni alisema kwamba ikiwa kuna mtu yeyote wa kulaumiwa kwa kukaa kwa Edday nchini Marekani, basi ni Seneta Karen Nyamu.

• “Hilo swali nenda kamuulize Karen Nyamu maana ni side chick ya Samidah sio mimi, kwanza nataka niweke wazi hili kwa wakenya wote wanaouliza kama mimi ndiye niliyemtoa Edday kutoka Kenya, sio mimi."

Mshawishi mahiri wa mitandaoni raia wa Kenya anayeishi Marekani Bernice Saroni amezungumzia kutengana kwa mwimbaji wa mugithi Samidoh Muchoki na Edday Nderitu na kushikilia kuwa hakuhusika katika jinsi mambo yalivyofanyika.

Katika mahojiano na wanablogu, Saroni alisema kwamba ikiwa kuna mtu yeyote wa kulaumiwa kwa kukaa kwa Edday nchini Marekani, basi ni Seneta Karen Nyamu.

Alipoulizwa kwa nini Edday alikataa kurudi nyumbani baada ya kuja Marekani kumtembelea, alisema:

“Hilo swali nenda kamuulize Karen Nyamu maana ni side chick ya Samidah sio mimi, kwanza nataka niweke wazi hili kwa wakenya wote wanaouliza kama mimi ndiye niliyemtoa Edith kutoka Kenya, mimi sio Karen. Iwapo Edith aliondoka Kenya na kwenda Marekani au uamuzi wowote aliofanya, mimi sihusiki na hilo. Kwa hiyo wanapaswa kukabiliana na Karen. Watu wasinihusishe na hilo," alisema.

Pia alikataa kujibu ikiwa amezungumza na binamu yake Samidoh kuhusu kurudiana na mke wake na akasema hayo ni maswala yao binafsi na hapaswi kuyaingilia.

Mama huyo wa watoto wanne pia alidai hana shida na seneta Nyamu, na kuongeza kuwa hajawahi kumkosea ili kumtaka asamehewe.

Nyamu na Edday, siku za nyuma, walitagusana mitandaoni wakimpigania mwimbaji  wa nyimbo za Mugiithi Samidoh.

Wakati fulani, walikaribia kupigana kihalisi huko Dubai, ambapo Nyamu alisafiri kwenda kukaa na Samidoh, ambaye hapo awali alikuwa amesafiri na mkewe.

Ikawachukua walinzi na marafiki wa karibu kumtoa Nyamu aliyekuwa amelewa mbali na Edday ambaye alikuwa akionekana kuchanganyikiwa na mwenye hasira.

Pia kuna wakati Nyamu alijitosa kwenye mitandao ya kijamii kumpiga Edday vijembe, akisema ndiye sababu ya kumwandikia ujumbe mrefu mumewe.

Hata hivyo, hivi karibuni,  Nyamu, alifunguka juu ya uhusiano wake wa kushangaza na alitumai kuwa siku moja, Edday atamkubali kama mke mwenza.

Alisema kuwa mpango wao wa kuwa na wake wengi umekuwa mkubwa kwa sababu wote ni watu mashuhuri, hivyo kufanya iwe vigumu kushughulikia mambo ya faragha.

"Nina imani, hata ikichukua mwaka, itafanya kazi. Kwa sababu moyo na nia iko mahali pazuri," alisema.