Kajala adadavua maelezo ya undani kuhusu mrithi wa Harmonize kwenye moyo wake

Kajala na Harmonize waliachana mwishoni mwa mwaka jana kimya kimya baada ya kupendana kwa muda mfupi tu.

Muhtasari

• “Mimi sijawahi kumfuata mwanamume, amenifuata yeye. Na mimi kwa sababu niliona niko tayari nikamkubalia,” aliongeza.

Image: INSTAGRAM// FRIDA KAJALA

Mwigizaji mkongwe wa Bongo Movie, Fridah Kajala Masanja ametangaza kwamba hivi karibuni mashabiki wake watarajie harusi yake nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari za mitandaoni, Kajala alisema kwamba alipata funzo kubwa kutokana na kuchumbiana na mtu maarufu – Harmonize – akisema kwamba ni kosa kubwa ambalo halitokuja kujirudia katika maisha yake.

“Siwezi kutaka mtu anayejulikana, kwa sababu nimeshamalizana na hayo mambo, nilitaka ni mtu ambaye namjua mimi na familia yangu. Ambaye ananifanya mimi niwe na furaha, hivyo tu,” Kajala alieleza sababu za kutaka mpenzi asiye celeb.

Pia muigizaji huyo mama wa binti Paula alijigamba kwamba katika maisha yake yote, hata siku moja hajawahi kumfuata mwanamume kumtongoza, akisema kwamba wengi akiwemo Harmonize na huyo ambaye anamficha wote walimfuata yeye tu.

“Mimi sijawahi kumfuata mwanamume, amenifuata yeye. Na mimi kwa sababu niliona niko tayari nikamkubalia,” aliongeza.

Alitoa vigezo vingi ambavyo vilimvutia kwa mpenzi mpya, akisema kwamba ni mambo makuu matatu lakini la tatu akalitaja kuwa siri yake.

“Ni mwanamume kamili, yule ambaye nilikuwa namhitaji, nina vigezo vyangu lakini kwangu mimi yule ni asilimia 100. Moja ni kutokuwa maarufu, pili anamcha Mungu na tatu ni siri yangu mwenyewe,” Kajala alieleza.

Kajala na Harmonize waliachana mwishoni mwa mwaka jana kimya kimya baada ya kupendana kwa muda mfupi tu.