Nyashinski aanguka jukwaani wakati wa hafla ya Solfest

Muhtasari

• Katika video ambayo imesambazwa mtandaoni, tukio hilo lilitokea alipokuwa akiingia jukwaani kutumbuiza kwa wimbo wake na Sauti Sol, `Short and sweet.

• "Nilijiingiza kwenye solfest kwa njia ya kipekee. Kipindi bora zaidi kuwahi kutokea,” 


Nyashisnki akitoa onyesho kwa solfest
Nyashisnki akitoa onyesho kwa solfest
Image: Insta

Rapa mashuhuri Nyashinski alijikwaa na kuanguka na kubingiria kwenye jukwaa alipokuwa akitumbuiza kwenye Solfest Alhamisi usiku.

Katika video ambayo imesambazwa mtandaoni, tukio hilo lilitokea alipokuwa akiingia jukwaani kutumbuiza wimbo wake na Sauti Sol, `Short and sweet`.

Bien alimwinua haraka na hafla ikaendelea vizuri huku mashabiki wakishangilia.

Nyashinski alipakia video kwenye Insta Story akiifanyia mzaha huku akitaja onyesho hilo kuwa bora zaidi kuwahi kutokea.

"Nilijiingiza kwenye solfest kwa njia ya kipekee. Kipindi bora zaidi kuwahi kutokea,” alinukuu video hiyo.

Onyesho hilo lilikuwa mwanzo wa densi  ya Sauti Sol kabla ya bendi hiyo maarufu kukamilisha  shughuli za onyesho hilo. Tamasha la Alhamisi lilikuwa onyesho la watu mashuhuri lililouzwa na tikiti ya Shilingi 20,000 kwa kila mmoja.

Bendi hiyo, mnamo Mei, ilitangaza kwamba wangeenda mapumziko, baada ya ziara yao ya ulimwengu ambayo ilihitimishwa mnamo Septemba 3. Hata  hivyo onyesho la Solfest linaashiria mwisho wa onyesho lao kama kikundi.

Onyesho lao la mwisho, lililopewa jina la Mashabiki show, litafanyika Jumamosi Novemba 4.

Mashabiki wa Nyashinski hata hivyo, walionyesha kufurahikia jinsi alivyojikwaa jukwaani na kutoa maoni  na hisia tofauti hasa baada ya kutazama video hiyo.

Njeri: "Sijawahi kuona mtu akipiga hatua ya kupendeza hivyo. Hadithi ya kweli."

Fancy Fingers: Bingwa wet !Hiyo ni kukuthibitisha kuwa uko sawa kabisaa bingwa, sasa Sato tutatesa zaidi.

Hata hivyo kuna wale ambao walichukulia tukio hilo kuwa kipindi wakisema ilikuwa njia mojawapo ya kuigiza na kuwafurahisha mashabiki.

" Huo ulikuwa mchezo mzuri sana na jinsi ulivyojiingiza. Niliupenda. Hata kuanguka kunaweza kuwa maridadi sana,"aliandika shabiki mmoja kwa jina la Anyiko.

" Hata akianguka anaanguka kibingwa,"aliongeza Wandera.