Burna Boy kuwalipa waandishi wa habari na bloggers ili kukoma kuandika kumhusu

Msanii huyo aliwataka wanahabari na wanablogu wote kufanya mkutano ili kujadili bei maalum atakayowalipa ili wakome kabisa kumtaja popote katika habari zao mitandaoni na kwenye vyombo vya habari.

Muhtasari

• Chapisho lake lilizua hisia tofauti, huku baadhi ya mashabiki wakimuonya kwamba "atasahauliwa" ikiwa wanablogu wataacha kubeba habari kumhusu.

Burna Boy
Burna Boy
Image: Instagram

Mwimbaji aliyeshinda tuzo ya Grammy, Damini Ogulu, almaarufu Burna Boy, ameeleza kuwa yuko tayari kuzilipa blogu za Nigeria kwa lengo moja tu - kuacha kutuma na kuandika habari zinazomhusu.

Nyota huyo aliyejiita "African Giant" alisema anafahamu kuwa hakuwa ameweka blogi yoyote nchini Nigeria hapo awali.

Alitoa wito kwa wanablogu nchini Nigeria kujadili bei na kumpitishia ili kuwasuluhisha waache kuchapisha habari zake "kabisa."

Kwenye akaunti yake ya X, awali ikijulikana kama Twitter mnamo Ijumaa, Burna Boy aliandika, "How far. wote hawa Instablog, PulseNg e.t.c, wanafanya mkutano wote kisha waamue ni kiasi gani nitawapa wote kuwafanya msahau jina langu kabisa. Najua sema sijawahi kulipa hata kabla kwa hivyo nasema fanya niendeshe mwishowe. Nawasalimu ndugu zangu!!”

Chapisho lake lilizua hisia tofauti, huku baadhi ya mashabiki wakimuonya kwamba "atasahauliwa" ikiwa wanablogu wataacha kubeba habari kumhusu.

Burna Boy na wanablogu wa Nigeria wana uhusiano mbaya kufuatia onyo lake kwa wanablogu dhidi ya kuchapisha muziki wake bila malipo kwenye tovuti zao.

Mwimbaji huyo wa ‘Last Last’ alikuwa amewasuta wanablogu wa Nigeria kwa kuvujisha muziki wake.

Taarifa hizo zinazoonekana kwamba zilimchukiza msanii huyo zinafuata siu chache tu baada ya kuonekana kwenye mazoezi ya freestyle na kufichua kaitka moja ya mishororo ya mashairi yake kwamba aliwahi kukataa shoo ya dola milioni 5 jijini Dubai baada ya kubaini kwamba hakuwa anaruhusiwa kuvuta sigara yake akiwa jukwaani.

Mwanamuziki huyo mashuhuri, anayejulikana kwa kutengeneza vichwa vya habari, alipendekeza mashirika ya vyombo vya habari yaitishe mkutano ili kujadili mpangilio maalum wa kifedha. Alieleza nia yake ya kuwalipa fidia kwa ushirikiano wao.