Rapudo amchukua Amber Ray kutoka klabuni usiku baada ya kusherehekea birthday

Katika picha za kipekee zilizonaswa na mwanablogu Vincent Mboya, Amber Ray alionekana akiondoka klabuni na kujiunga na Rapudo katika gari lake aina ya Range Rover kabla ya kuondoka pamoja.

Muhtasari

β€’ Wawili hao waliondoka pamoja ndani ya gari licha ya kuwepo kwa uvumi kwamba waliachana mwezi jana.

KENNEDY RAPUDO WAKIWA NA AMBER RAY. PICHA INSTAGRAM
KENNEDY RAPUDO WAKIWA NA AMBER RAY. PICHA INSTAGRAM

Unaambiwa mambo ya watu wawili waliowahi kushiriki kitanda kimoja wakiwa uchi achana nayo kabisa.

Maoya yaliyomo mjini ni kwamba Amber Ray na mpenzi wake Kennedy Rapudo wameonesha dalili zote kwamba wapo pamoja licha ya awali kuigiza mitandaoni kuwaaminisha mashabiki wao kwamba wameachana.

Novemba 4, Amber Ray alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na katika kile ambacho hakikutarajiwa, Kennedy Rapudo alikwenda mitandaoni na kumuachia ujumbe mtamu akimshukuru Mungu na hatima kwa kuwakutanisha.

Rapudo alikwenda mbele na kumtaka Ray kuingia katika klabu yoyote ya chago lake ili kuitisha vinywaji ghali kisha baadae yeye kama tajiri atumiwe bili.

"Wakati ulimwengu ulituleta pamoja, lilikuwa jambo bora zaidi ambalo limewahi kunipata. Nakutakia siku njema ya kuzaliwa bado. Happy birthday mama @africanahrapudo πŸŽ‚πŸŽŠπŸŽ. Shampeni ya pop 🍾🍾 watumie tajiri bill,” alinukuu picha za Amber Ray ambaye alikuwa amevalia gauni jeusi.

Amber bado hajajibu ujumbe wa Rapudo ingawa aliacha kumfuata baada ya kuachana.

Ikiwa hiyo haitoshi, wakati Ray yuko klabuni akiserereka na marafiki zake, Rapudo alitokea hapo akiwa na gari lake la kifahari usiku wa manane.

Katika picha za kipekee zilizonaswa na mwanablogu Vincent Mboya, Amber Ray alionekana akiondoka klabuni na kujiunga na Rapudo katika gari lake aina ya Range Rover kabla ya kuondoka pamoja.

Uhusiano wa Amber na Rapudo ulikwenda kusini kuelekea katikati ya Oktoba kutokana na tukio la shambulio lililotokea wakati walevi. Wakati akishiriki kuhusu suala hilo, alisema kwamba aliamua kuchagua mwenyewe.

"Najua itakuwa siku/wiki ndefu kwangu, lakini ningependelea kuwa na amani ndani kuliko kutarajia kimbilio la uwongo kwa nje. Afadhali niseme ukweli wangu kuliko kuruhusu uvumi kuharibu kile ambacho nimejenga kwa ajili yangu na familia yangu hadi sasa. Mambo katika kaya yangu hayajakuwa sawa… lakini yatakuwa sawa. Familia yangu itakuwa sawa. Na hatimaye, nitakuwa sawa,” Amber alisema kwenye Instagram.

"Ni tukio ambalo halipaswi kutokea na ninajuta sana na kwa majuto makubwa kwamba ilitokea kwa mtu ambaye niliapa kumlinda na kumpenda kwa yote niliyokuwa nayo," Rapudo alisema kwa upande mwingine.

Aliongeza kuwa tukio la pekee halipaswi kumtaja kama mtu mwenye jeuri.