Actress Nyaboke akutana na DJ Euphorique, atania uhodari wa walemavu kwenye mapenzi

Nyaboke alisema uvumi mitaani ni kwamba watu wenye ulemavu mara nyingi huwa wazuri sana katika shughuli za chumbani.

Muhtasari

• "Sitakaa single hapa nje na huyu anataka kunioa.mshone vitenge aisay,” aliandika kwa utani.

Nyaboke na DJ Euphorique.
Nyaboke na DJ Euphorique.
Image: Facebook, Instagram

Muigizaji wa zamani wa Tahidi High, Gloria Moraa Nyaboke amezua utani mitandaoni baada ya kupakia picha alipokutana na aliyekuwa DJ rasmi wa kwaya ya ikulu enzi za Uhuru Kenyatta, DJ Euphorique.

Nyaboke kupitia ukurasa wake wa Facebook alipakia picha hiyo na kwa utani akawasuta baadhi ya mashabiki wake ambao walilenga kuandika komenti mbaya kuwa sasa ameanza kuchumbiana mpaka na watu wenye ulemavu.

Nyaboke alizidisha utani akisema kwamba hawezi kaaa single muda mrefu hivyo wakati watu kama DJ Euphorique wako na wamebarikiwa, huku akiwatania mashabiki wake kujiandaa kwa kushona vitenge.

Najua mtaanza kusema ati "ooh sai anakula mpaka vilema"....let me tell you Maina.....huyu atajua huruma ni estate,nakula mpaka ile anapewa na serikali..sasa bado kipofu na mtu asini advice...sitakaa single hapa nje na huyu anataka kunioa.mshone vitenge aisay,” aliandika kwa utani.

Mwigizaji huyo anayejiita gaidi mkuu aliendela kusema kwamba hajawahi chumbiana na mtu mwenye ulemavu lakini akadokeza kwamba uvumi uliopo mitaani ni kwamba watu kama hao mara nyingi huwa wazuri sana katika shughuli za chumbani.

“Hakuna pesa chafu value ni ile.ubaya sasa mimi ndio ntashinda juu kwa hii relationship. Mniombee @djeuphorique stock energy drinks. Lakini naskia hawa watu wanaweza kulima uzimie,” alimaliza.

DJ Euphorique alijulikana na wengi baada ya kuteuliwa na rais mstaafu Uhuru Kenyatta kama DJ rasmi wa kwaya ya ikulu lakini baada ya hatamu zake kumalizika, haiku wazi iwapo DJ huyo bado aliendelea kuhudumu chini ya uongozi wa Ruto au la.