Diamond kutambulisha msanii mpya wa WCB mwezi huu wa Novemba, atangaza tarehe!

Aliwapa matumaini makubwa mashabiki wake akiwaahidi kwamba hatakuwa msanii hivi hivi bali ni jina kubwa na mwenye talanta ya kupigiwa mfano

Muhtasari

• Kupitia ukurasa wake wa X, awali ukijulikana kama Twitter, Diamond alitoa tangazo hilo kwa maneno machache akiandika pia tarehe.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Mkurugenzi mtendaji wa lebo ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz ametangaza kumtambulisha msanii mwingine mkubwa katika lebo hiyo kabla ya mwezi huu wa Novemba kukamilika.

Kupitia ukurasa wake wa X, awali ukijulikana kama Twitter, Diamond alitoa tangazo hilo kwa maneno machache akiandika pia tarehe ambazo msanii huyo atazinduliwa rasmi katika sherehe kubwa itakayochukua siku mbili kumtambulisha.

Aliwapa matumaini makubwa mashabiki wake akiwaahidi kwamba hatakuwa msanii hivi hivi bali ni jina kubwa na mwenye talanta ya kupigiwa mfano, kwani siku zote Wasafi huwa si wa kubahatisha linapokuja suala la kusaini wasanii.

“Nov 16th / 17th 2023, tunamtambulisha SUPER STAR mpya, Msanii Mpya wa WCB WASAFI!!! Tunaanza Rasmi Siku Zilizosalia Kuanzia Kesho! #Wcb4Life #Wasafi” Diamond aliandika X.

Tangazo hili linaenda kinyume na tangazo ambalo alifanya mapema mwezi Julai alipokuwa akitoa tahadhari kwa wasanii wenzake kuhusu kuachia miziki kwa mfululizo hadi mwakani.

Akitoa tangazo hilo, Diamond alikuwa amedokeza kwamba angemtambulisha msanii mpya kwenye lebo ya Wasafi mapema Januari mwaka 2024, muda ambao angempisha msanii huyo kuchukua hatamu ya kuongoza kwenye trend baada ya yeye kufanya hivyo kuanzia Julai hadi Desemba mfululizo bila kutikiswa.

“Januari 2024 nitampisha msanii wangu mpya,” Diamond alisema.

“Haimanishi eti ndio kupuuza kanisa kufanya ngoma na rafiki zangu tokea Tanzania ama East Africa. Nazo zina umuhimu kwa waswahili wenzangu haswa msimu kama huu wa Wasafi Festival unavyokuja. Hivyo tegemeeni pia kumwagika kwa nyingi tu za kutosha,” Diamond alisema.