Nilifeki kupata ajali nikatumiwa shilingi 256K kutoka kwa wanaume 30 - Risper Faith afichua

“Msinihukumu, ni kutafuta pesa kusema kweli, hata nyinyi najua pia mmefanay vituko kupata pesa.Mimi nilikuja Nairobi kutafuta pesa sikuja kuteseka," alisema akijitetea.

Muhtasari

• "Bili niliandikiwa na yule daktari ni elfu 56."

• "Wale wababa wangu wakatuma kila mmoja kiasi tofauti tofauti na hivyo tu nilijikuta nimechangisha 256k,” aliongeza.

Lady Risper
Lady Risper
Image: Instagram

Mwanasosholaiti wa muda mrefu Risper Faith maarufu kama Lady Risper amewashangaza mashabiki wake baada ya kuhadithia moja ya visa vya kijanja ambavyo alikuwa anavitumia ili kupata pesa bila jasho kabla ya kuolewa na kutulia katika ndoa.

Risper alikuwa live kwenye Instagram yake ambapo aliamua kutema nyongo ya siri ambayo ameiweka kwa muda mrefu.

Alisema kwamba kipindi kimoja alilazimika kufeki kupata ajali na hata kuwalipa madaktari hospitalini kumruhusu kulalia kitanda katika chumba cha dharura ili tu kupiga picha na kuwatumia wapenzi wake kama njia moja ya kuwatoza pesa.

Kwa maneno yake, Risper alihadithia akisema;

“Niliendesha gari tukaenda all the way to Nakuru, sasa on the way tulikutana na ajali… eeh aki Mungu nisamehe, vitu tunafanya ili kupata pesa ni vingi sana…lakiji sikutoka Webuye kuja Nairobi kuteseka, nilikuja kutusua kimaisha. Sijaja kucheka au kufurahisha mtu, nimekuja kutafuta pesa,” alianza.

“Kufika hapo karibu na hospitali moja, tulipata hapo ajali, yaani tuliona gari limepata ajali, nikaenda nikapiga picha kwa hiyo gari halafu kuna damu ilikuwa hapo nikachukua nikajipaka uso na kichwa nikajipiga picha. Wakati huo niko na orodha ya wababa kwa simu yangu…”

“Msinihukumu, ni kutafuta pesa kusema kweli, hata nyinyi najua pia mmefanay vituko kupata pesa. Haya, kutoka hapo nikaenda kwa hiyo hospitali nikahonga daktari alikuwepo mdogo hivi shilingi elfu 3 ili aniwekee sindano ya damu bila damu na kunilaza kweney kitanda cha chumba cha dharura…”

“Tukatoka hapo tuakelea tulikokuwa tunaenda na nikatumia wababa kama 30 zile picha nikawaambia nilipata ajali nikielekea Nakuru. Bili niliandikiwa na yule daktari ni elfu 56. Wale wababa wangu wakatuma kila mmoja kiasi tofauti tofauti na hivyo tu nilijikuta nimechangisha 256k,” aliongeza.

Aliporudi Nairobi, alipata bandeji za uwongo, na wanaume walikuwa wakija na kumtembelea na kumletea chochote alichoomba ambacho alilazimika kuweka chakula.

Aliporudi Nairobi, alipata bandeji za uwongo, na wanaume walikuwa wakija na kumtembelea na kumletea chochote alichoomba ambacho alilazimika kuweka chakula.