Shakib amtuma mtangazaji aliyekwenda kumhoji Zari kumuuliza ni lini atamzalia mtoto

Mtangazaji huyo alisema kabla ya mahojiano yake na Zari alikutana na mumewe, Shakib na moja ya swali ambalo yeye [Shakib] alimtaka kuuliza Zari ni kuhusu lini atamzalia.

Muhtasari

• Remmy alisema hata hivyo mashabiki wa Zari walichukulia swali hilo kama suala la kufa na kupona na kuanza kumkoromea mitandaoni.

• Alisema amekuwa akipokea matusi wengi wakimuita tasa kwa vile hana mtoto licha ya kuulizia wanawake wengine kuhusu mtoto.

amemsherehekea mke wake Zari Hassan.
Shakib amemsherehekea mke wake Zari Hassan.
Image: INSTAGRAM// SHAKIB CHAM

Mtangazaji wa runinga nchini Uganda amejitetea baada ya kumkabili Zari na maswali magumu kuhusu ndoa yake na kijana mdogo Shakib Cham Lutaaya likiwemo suala la ni lini atamzalia mtoto.

Kwa mujibu wa blogu za kutoka taifa hilo jirani, mtangazaji Remmy Precious anayeongoza kipindi cha Uncut kwenye runinga ya Sanyuka TV, alimuuliza Zari swali hilo ambalo halikukaa vizuri kwa upande wa mjasiriamali huyo mwenye biashara nyingi Afrika Kusini.

Lakini kwa kujitetea baadae baada ya shoo, Mtangazaji huyo alijitetea akisema kwamba hakufanya vile kwa kutaka kumkomoa Zari bali swali hilo alitumwa na mumewe, Shakib kujua ni lini atamzalia mtoto.

“Sikuwahi kupanga kuuliza swali hilo. Ni mume wake kabla ya onyesho, ambaye aliniambia niulize. Kwa kweli yeye (Zari) aliniona nikipanda na kushuka naye akaniuliza nini kinaendelea,” alisema.

"Pia alikusudia kwa njia ya mzaha na nikamuuliza kwa upole na heshima, naye akajibu kwa raha."

Mtangazaji huyo mapema wiki jana aligonga vichwa vya habari baada ya kutiririkwa na machozi akishiriki mkutano na wanablogu.

Katika mkutano huo, alilia akisema kwamba tangu mahojiano yale na Zari, wengi wamekuwa wakimburuza mitandaoni wakimsuta kwa nini hajapata mtoto wake mwenyewe hali ya kuwa anashinda akiwauliza wanawake wengine katika mahojiano runingani.

“Watu wanaosema mimi ni tasa… Lakini mimi si Mungu. Sijui ni lini nitazaa. Hakuna mwanamke aliyeolewa maishani ambaye hataki kuzaa,” alisema.

"Najua unataka nishati hasi kila wakati, lakini baadhi ya mambo tunapaswa kujificha….Ninaomba na ninajua kwamba siku moja Mungu atanibariki na mtoto," alisema kabla ya kuvunjika moyo.