•Meneja huyu aliyejitabulisha kwa jina Ding'ano amesimulia kuwa ni kweli Harmonize alitapeliwa pesa hizo na kesi tayari inaendelea Mahakamani
Menaja wa staa wa Bongo amejitokeza na kunzugumzia swala la Bosi wake kudai kuibiwa shilingi billioni saba alizowekeza hili kufungua vituo vya habari.
Kupitia mahojiano ya Moja ya moja meneja wa Harmonize amejibu madai kwenye mitandao kuwa Utajiri wa msanii Harmonize haufiki billioni saba.
Meneja huyo kwa jina Ding'ano amesimulia kuwa ni kweli Harmonize alitapeliwa pesa hizo na kesi tayari inaendelea Mahakamani.
"Harmonize ni tajari mno mfumo wake wa kupata hela ni wajuu sana wengi wanakana hilo wakisema Harmonize hanauwezo wa kumiliki billioni saba ila Harmonize ni tajiri wa zaidi ya billioni saba,"alisema.
Meneja alifunguka na kusema kwamba utajiri wa Harmonize ni wa juu akizungumzia magari ya thamani aina ta Range Rover na kumiliki magari saba aina ya V8.
Staa huyu wa bongo Harmonize alisimulia hayo wakati alipokuwa nchini Kenya mwishoni mwa wiki. Hramonise alisema alikuwa ametenga kaiasi fulani cha pesa kwa lengo la kufungua vituo vya habari ya lebo ya konde.
Ni Siku tu chache baada msanii Diamond Platnumz kukiri kutapeliwa shilingi billioni nne za Tanzania alizoekeza kununua ndege ya kibnafsi.
Staa huyo wa Bongofleva, amekiri alipoteza pesa hizo alizokuwa amepangia kufungua nazo nyumba ya habari ya lebo ya konde.