Milly Chebby amezungumza baada ya watu kwenye Instagram kudai kuwa anafanana sana na aliyekuwa rafiki yake wa ndani Jackie Matubia.
Chebby alikuwa amepakia picha zake kadhaa za hivi punde wakati mashabiki wake waligundua kuwa anafanana na Jackie katika mojawapo ya picha hizo.
“Aki na si uchokozi, picha ya kwanza unakaa JMatubia.Lakini unapendeza,” aliandika mtumiaji mmoja wa Instagram.
Milly alikejeli maoni hayo na kusema kwamba walikuwa na sura zinazofanana kwa sababu wao ni mandungu.
"Ni kwa sababu sisi ni mandugu," alijibu.
Shabiki mwingine alisema, "Sawa, lakini nilidhani ni Jackie mwanzoni, nadhani nimeangalia kwa kasi."
Pia alijibu maoni hayo akimhakikishia shabiki huyo kuwa ni yeye na si rafikiye wa zamani.
Mashabiki hao waliendelea kutoa maoni wakisisitiza kufanana kwa hao wawili.
"Nilidhani ni yeye kweli. Amemfanana.”
"Unakaa Jackie sana."
Jackie na Chebby kwa sasa hawana uhusiano mzuri kama hapo awali. Mashabiki walikuwa na uhakika kwamba urafiki wa wawili hao umetokomea baada ya kuacha kuaandaa maudhui na kujumuika pamoja.
Hata hivyo, hapo awali Chebby na Matubia walikuwa wamezima madai ya kutoelewana.
Uthibitisho wa uhusiano wao wenye matatizo ulikuja wakati Jackie alipokosa kuhudhuria sherehe ya harusi ya kitamaduni ya Milly na mumewe.
Mashabiki walipotafuta maoni na hisia za Jackie, alisema kwamba wao (bila kutaja mtu yeyote haswa) walisema kwamba hana mume na alikuwa na moyo mbaya.