DJ mmoja ambaye alishirikishwa kwenye video ya Ameyatimba Remix yake Whozu, Billnass na Mbosso amefichua kwamba msanii Diamond Platnumz hakuwa ‘ameibariki’ video hiyo kabla ya kutoka.
Akizungumza na blogu moja nchini humo baada ya BASATA kuamuru video hiyo kushushwa nakutoa adhabu kali kwa wasanii husika, DJ Msabato alisema kwamba Diamond alikuwa amepinga vikali kuachiliwa kwa ngoma hiyo lakini wasanii hao watatu walifanya kulazimisha tu.
“Hii video tuliifanya muda mrevu nyuma kama miezi miwili mitatu nyuma lakini kutokana na matamasha ikawa imechelewa kutoka. Pia niliambiwa kwamba biggie [Diamond] alikuwa amekataa kama mara mbili au tatu hivi isitoke, lakini sijui kwa nini ikawa imetoka,” DJ Msabato alisema.
DJ huyo alikwenda kwa undani Zaidi kufichua kwa nini pengine anahisi Diamond alikuwa anapinga kuachiliwa kwa ngoma hiyo.
“Kuna baadhi ya scenens zilikuwa si nzuri, za Mbosso kwa sababu kuna zingine za kitanani zilipunguzwa zile za kitandani. Kwa hiyo naona hiyo nayo ilichangia kupunguzwa na pengine Diamond kuikataa,” aliongeza.
Baada ya wasanii hao kutoa video hiyo kinyume na matakwa ya Diamond, DJ Msabato ambaye anafanya kazi katika kituo kimoja cha redio anasema walipoiona hawakutana kuongea hewani lakini pembeni waliteta na kutabiri kwamba ingekuja kuleta matatizo ya kimaadili na BASATA.
Alisema kwamba scenes zilizoleta ukakasi ni kuonekana kwamba amebakwa mtu na akahisi pengine mwishoni kungeandikwa kwamba hawaungi mkono vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na kuweka wazi kwamba chochote kilichoonekana kwenye video si kweli bali ni maigizo tu.
Ikumbukwe wikendi tuliripoti kwamba BASATA iliwafungia wasanii hao kati ya miezi 3 hadi 6 kutojihusisha na kazi yoyote ya Sanaa lakini pia kila mmoja kutozwa faini ya milioni 3.