Mchekeshaji Eric Omondi ameazisha mchakato wa kuchangisha pesa hili kupumzisha mwili wa mwanaume mmoja ambaye alifariki mwaka wa 2019 huku mwili wake ukiripotiwa kukaa mochwari kwa miaka tano.
Kulingana na ujumbe kwenye mtandao wake wa instagram Marehemu Eric Gori alifariki mwaka wa 2019 na mwili wake hadi leo bado umo kwenye chumba cha kuifadhi maiti katika makafani ya Chiromo.
Eric amesimulia zaidi kwamba marehemu aliacha watoto wawili akisema kuwa familia yake imevumilia kwa miaka tano kwa kukosa hela za kumzika mpedwa wao.
"Nimewasiliana na wahudumu wa makavani ya Chiromo na kuwajulisha ili kutayarisha mwili wa marehemu ili tuweze kumpumuzisha jumatano iwapa tutafanikiwa kuchangisha zaidi ya laki saba zinazohitajika hili kuruhusiwa kuchukua mwili,"alisema Eric Omondi.
Mchekeshaji Eric amesema kuwa iwapo watafanikiwa kumzika marehemu ataanzisha tena mchakato wa kuchanga hela ili kulipia karo watoto wawili walioachwa na marehemu.
Mchango huyo unatokea siku chache baada ya mwanablogu huyu kuonekana hivi majuzi akimsaidia mama aliyepoteza mtoto wake kumzika katika makaburi ya Langata.