•Msanii huyo kwa kauli yake alimsifu Vera Sidika akisema iwapo angepata nafasi ndiye mwanadada wa Kenya ambaye siku zote angemchangua kama mpenziwe.
Staa wa Bongo, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amefunguka kwa kusema kuwa mwanasosholaiti Vera Sidika ndio mwadada nchini Kenya anyeweza kumchumbia iwapo angeaza kuchumbiana nchini.
Msaanii huyo maarufu nchini Tanzania alisema hayo wakati alipokuwa akitumbuiza wafuasi wake wa Kenya katika eneo moja la burudani mjini Thika.
Harmonize alifunguka hisia zake kwa Vera Sidika wakati alipokuwa akiwasifu wanadada wa Kenya waliokuwa wakinengua viuno huku wakimshabikia alipokuwa akitumbuiza jukwaani.
"Mara kwa mara mimi hujiuliza kwanini sijawahi chumbia warembo wazuri wa Kenya,kumbe nakosa mengii aaaaah...kuna manzi mmoja wa Nairobi nammezea sana siku nitalewa nitasema ni nani ....kuna mtu ameniambia Vera Sidika hana mchumba ni kweli,"aliuliza.
Msanii huyo kwa kauli yake alimsifu Vera Sidika akisema iwapo angepata nafasi ndiye mwanadada wa Kenya ambaye siku zote angemchangua kama mpenzi wake.
Harmonize alikuwa nchini Kenya kwa ziara ya siku mbili kwa tamasha moja ambalo aliwatumbuiza wafuasi wake,huku akisema kuwa mji wa Nairobi ndio moja kati ya miji mikuu amepata nafasi ya kutumbuiza mara nyingi.