Baba levo azungumza baada ya Diamond kumzawadi mtoto wake gari

Diamond Platnumzs ndio babu wa mtoto wangu Baba levo asema

Muhtasari

•Msanii huyo ambaye mara nyingi kwenye mahojiano humtaja Diamond kama babake wakati wa mahojiano hayo alitoa kauli akisema kuwa Diamond alimnulia mtoto wake gari kwa kuwa ni babu yake

Image: INSTAGRAM// BABA LEVO

Msanii wa Tanzania, Revokatus Kipando, almaarufu Baba Levo,amejitokea hadharani na kusimulia furaha yake huku akionesha gari la  kifahari ambalo alisema kuwa lilinunuliwa na msanii Diamond Platnumzs kwa ajili ya mtoto wake.

"Nina furaha sana hata baada ya msanii Diamond kulaghaiwa Billioni  4 ana huwezo wa kununulia mtoto wangu Gari la kifahari ya zaidi ya millioni mbili na nusu,gari hilo amelinunua kwa ajili ya mtoto wangu kutembelea anapopelekwa kliniki,"alisema.

Msanii huyo ambaye kwa mara nyingi kwenye mahojiano humtaja Diamond kama babake wakati wa mahojiano hayo alitoa kauli akisema kuwa Diamond alimnunulia mtoto wake gari kwa kuwa ni babu yake.

"Mtoto wangu amenunuliwa gari ili na babu yake Diamond Platnumzs hili wakati anaposafiri awe kwa gari nzuri", alisema Baba levo.

Haya yanajiri siku chache baada ya Msanii almaarufu Baba Levo, kuwashagaza wengi baada ya kufunguka wazi akisema kwamba anamchukulia Diamond kama Babake mzazi na anataka awekwe  kwenye urithi wa mali yake.

Kwenye mahojiana  msanii  huyu aliongeza kuwa yeyote anayekerwa na jambo hilo aelekee mahakamani kumshtaki kwani Diamond ndio mzazi anayemsaidia kwa maisha yake.

 

 

 

.