logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond amekuwa akitaka kukutana na Harmonize ili azungumze naye - Baba Levo afichua

Harmonize aliondoka 2019 huku Rayvanny akiondoka 2022.

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 November 2023 - 08:36

Muhtasari


  • • Harmonize aliondoka WCB mwishoni mwa 2019 kwa njia ya kisjhari iliyovunjilia mbali uswahiba wake na Diamond kiasi kwamba hawaonani hadi leo hii.
katika picha ya maktaba.

Chawa mkubwa wa WCB Wasafi, Baba Levo amefichua kwamba bosi wake Diamond Platnumz kwa mara kadhaa amekuwa akifanya juhudi za kukutana na aliyekuwa msanii wake Harmonize ili kufanya mazungumzo naye.

Baba Levo alikuwa anazungumza na waandishi wa habari za mitandaoni baada ya kutambulisha gari jipya alilosema kwamba alisaidiwa kununua na Diamond kwa ajili ya mwanawe mchanga ambaye alitangaza siku chache zilizopita kwamba anaitwa Platnumz.

Baba Levo aliulizwa kuhusu picha ya pamoja ambayo alionekana amepigwa akiwa na Harmonize na Rayvanny kwenye casino.

Alifichua kwamba Harmonize muda wote hana baya na bosi wake wa zamani, Diamond Platnumz na pia kukiri kwamba Diamond ameshawahi kumwambia kwamba angependa sana siku moja kukutana na wasanii Harmonize na Rayvanny kwa ajili ya maongezi ya kile alikiita ushauri.

“Mimi sioni kama Harmonize ana tatizo lolote nimekaa naye nimeongea naye, na nimekaa tena na Diamond Platnumz. Diamond ashawahi kuniambia mimi kwamba bwana siku moja atakaa na hao vijana wake wote [Harmonize na Rayvanny], pamoja awape ushauri namna ambavyo wanaweza kukanyaga kwa sababu anaona wametoka ndani ya lebo lakini hawafiki ile level ambayo yeye alikuwa amepanga kwenye kichwa chake wakiwa ndani ya lebo,” Baba Levo alisema.

Baba Levo alisisitiza kwamba huo si utani bali ni kitu ambacho Diamond amemuambia mara si moja kwamba anatakani sana kukaa siku moja na hao vijana ili kuwamegea ushauri wa kutusua kimuziki.

Chawa huyo alisema kwamba jukumu la watatu hao kukutana, ikizingatiwa kwamba Harmonize na Diamond ni kama paka na panya wasioweza kuonana, yeye ndiye atafanikisha mkutano wao.

“Mimi ndio nitawaleta, Diamond anajua kwamba kuna wengine wana kinyongo na chuki lakini anajua hawawezi kumwepuka kwa sababu yeye ni baba yao. Kwa hiyo nitawaleta, watakaa naye atawashauri,” aliongeza.

Harmonize aliondoka WCB mwishoni mwa 2019 kwa njia ya kisjhari iliyovunjilia mbali uswahiba wake na Diamond kiasi kwamba hawaonani hadi leo hii.

Kwa upande wake, Rayvanny alitangaza kuondoka WCB mwaka jana, lakini kinyume na Harmonize, yeye aliweka mambo sawa na kupewa Baraka za babake kwenye muziki [Diamond] na hata baada ya kuondoka, wawili hao wamekuwa wakishirikiana kwa kazi za muziki licha ya kwamba hawana ule ukaribu kama wa zamani akiwa chini ya lebo ya WCB.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved