Eric Omondi asema bintiye alipata pasipoti akiwa wiki mbili

Mtoto wangu ni Malkia ndio maana anaweza kusafiri mataifa yote alisema Omondi

Muhtasari

•Mtoto ambaye alikuwa gumzo mitaani baada ya Eric kusema angelipisha zaidi ya millioni 50 kwa yeyote angetaka kumuona mtoto huyo

ERIC OMONDI NA MPENZIWE LYNNE NA MTOTO WAO

Mcheshi na mwanablogu Eric Omondi amemyeshea sifa tele  bintiye Kaylar huku akifunguka kuwa wiki mbili tu baada ya kuzaliwa bintiye alikuwa na pasipoti ambayo anaweza kutumia  kusafiria mataifa yote.

"Mtoto wangu ni 'malkia' alikuwa baraka nyingi kwangu ndio maana kama baba nilihakikisha  kuwa amepata pasipoti wiki mbili baada ya kuzaliwa kwani malkia anafaa kusafiri kwa nchi zote," alisema Omondi.

Hata hivyo mchekeshaji huyo alisimulia zaidi akisema kuwa bintiye kwa sasa amefikisha umri wa miezi mitatu akitaja kuwa anafurahia kukua kwake jinsi alivyo mrembo na mpole akisema kuwa mtoto huyo amefanya aheshimike kote.

Miezi  mitatu iliyopita mchekeshaji Eric Omondi na mpenzi wake wa muda mrefu Lynn  walikuwa na hamu ya kutarajia mtoto wao wa kwanza miezi michache baada ya kutangaza kuharibikiwa na mimba yao ya kwanza.

Wanandoa hao walitangaza mnamo Julai 22, 2023 kwamba walikuwa wanatarajia mtoto wa kike katika familia yao.

Mtoto ambaye alikuwa gumzo mitaani baada ya Eric kusema angelipisha zaidi ya millioni 50 kwa yeyote angetaka kumuona mtoto huyo.