Msanii wa Kenya almaarufu KRG The Don amepinga vikali mchango wa Youtuba Mr Beast aliyedaiwa kuchimba visima 52 akisema kuwa Youtuba huyo alikuwa akicheza na akili za Wakenya hili kupata Wafuasi wengi Kwenye mtandao.
"Mr Beast alikuja Kenya kuunda maudhui ya chaneli yake wale si kusaidia kwa sasa amecheza na akili za Wakenya mpaka akafikisha wafuasi millioni 70 kwa mtandao wake kwa kucheza na fikra za watu,"alisema KRG.
Msanii huyo alisema hayo baada ya kuchapisha video moja Kwenye mtandao wake huku akimtaka Mr Beast kuacha kuchezea fikra za wakenya ili kupata wafuasi.
"Kusaidia hutoka kwa roho ya kila mwanadamu,si kwa kuchezea fikra za watu ili kujifanya uko na roho ya kusaidia, kujitafutia jina ili kujinufaisha kwa kupata wafuasi wengi,"alisema.
Msanii huyo aliwataka wafuasi kwenye mitandao pia kukoma kumtaja ajitokeze kusaidia wakenya kama alivyofanya Youtuba huyo wa Marekani Mr Beast.
Kila mkenya afanye maendeleo yake kivyake maisha ni ngumu kwa kila mkenya mambo ya kunitaka kujitokeza kusaidia mkome kusaidia ni uamuzi wa mtu si kulazimishwa,"alisema.
Msanii huyo, anayejulikana kwa kuwa muazi na mtindo wake wa maisha, alisema kuwa utajiri wake si kwa ajili ya kufanya nia njema kama bilionea huyo wa Marekani. Aidha alifichua kuwa hana huruma kwa watu ambao hawako tayari kujiondoa kutoka kwa umaskini.