Wahu azugumzia safari yake kama mlezi wa watoto watatu

The Mathenges, kama wanavyojiita wasanii hao (Wahu na Nameless) waliadhimisha miaka 18 katika ndoa mwaka huu.

Muhtasari

•Nina mtoto wa miaka kumi na saba,wa pili miaka kumi na kitinda mimba wangu ni mwaka mmoja na mwezi ,

• Watoto hao wote kila mmoja  ana mahitaji yake maalum, huwalea ili wawe na maisha mazuri kuliko yangu,'alisema.

Nameless na Wahu
Nameless na Wahu
Image: Facebook

Mwanamuziki maarufu wa Kenya Wahu Kagwi amemshukuru Mungu kwa baraka, kumfanya kuwa mama mlezi wa watoto watatu na ndoa ya miaka kumi na minane

"Wengi huniuliza safari ya kulea iko aje?,ila kwangu ni neema kubwa kuwa ndani ya ndoa kwa miaka 18, kuwa mama wa watoto watatu mlezi ya miaka 17 ni jambo ambalo mimi hujivunia na kushukuru Mungu kwa upendo  kwa familia yangu," alisema Wahu.

Mwanamuziki huyo alisimulia zaidi, kuwa mama wa watoto watatu ni jambo ambalo humfurahisha. Alisema yeye wanawe ni marafiki mno jambo ambalo limemsaidia sana kujua changamoto wanazopitia.  

"Nina mtoto wa miaka kumi na saba,wa pili miaka kumi na kitinda mimba wangu ni mwaka mmoja na mwezi ,watoto hao wote kila mmoja  ana mahitaji yake maalum, huwalea ili wawe na maisha mazuri kuliko yangu,'alisema.

Wahu aliongeza kuwa cha muhimu katika ndoa ni kuwa na upendo kwa watoto na familia nzima.

 

Hayo yanajiri siku chache baada ya The Mathenges, kama wanavyojiita kuadhimisha miaka 18 pamoja kwa safari ya ndoa.