Rick Ross kuajiri mhudumu wa ndege yake ya kibinafsi, mshahara milioni 17 kwa mwaka (video)

"Ni lazima uwe na uzoefu, uwe mchangamvu na uwe vizuri katika kumhudumia Ross…” Msanii huyo alisema.

Muhtasari

• Ross alisema kwamba kwa kawaida kuzunguka katika maeneo mbali mbali kote ulimwenguni kumekuwa moja kati ya biashara zake nyingi.

Rick Ross.
Rick Ross.
Image: Instagram

Rapa Na Mfanyabiashara Kutoka Marekani Rick Ross Ametangaza Kuajiri Mhudumu Wa Ndege  Atakayefanya Kazi Kwenye Ndege Yake ya kibinafsi, ambapo atamlipa hadi kiasi cha shilingi milioni 17 pesa za Kenya kwa mwaka [dola 115,000].

Tajiri huyo mmiliki wa ndege za Bel Air alitangaza hili katika video moja ambayo imeenezwa mitandaoni ambapo amesema kwamba anatafuta mhudumu mwenye ucheshi na umahiri wa juu katika kufanya kazi yake.

“Niaje, huyu ni bosi mkubwa kwenye kaya, hapa nyuma yangu ni ndege yangu ya Bel Air. Bosi Rick Ross anatafuta mhudumu wake wa kibinafsi katika ndege yake ya kibinafsi. Mshahara ni kati ya dola elfu 85 hadi dola elfu 115 kwa mwaka. Ni lazima uwe na uzoefu, uwe mchangamvu na uwe vizuri katika kumhudumia Ross…” Msanii huyo alisema.

Ross alisema kwamba kwa kawaida kuzunguka katika maeneo mbali mbali kote ulimwenguni kumekuwa moja kati ya biashara zake nyingi na hivyo kuona haja ya kupata mhudumu wa kibinafsi.

Alimalizia kutoa barua pepe yake na kusisitiza kwamba maombi ya kazi atakayoyapokea ni kutoka kwa waombaji wasio wa mzaha pekee.