Hatimaye Diamond amtambulisha msanii mpya kwenye Lebo lake la Wasafi

D VOICE alisimulia furaha yake na kumtaja Diamond kuwa baba mlezi wa nyota nyingi za wanamuziki wanaochipuka.

Muhtasari

•Diamond alisimulia kuwa nia yake kwa Kumtabulisha Msanii D VOICE ni kumlea kama mwanamziki na kuchipua nyota yake kwani ni mwanamuziki mchanga mwenye bidii na heshima

Diamond na DVoice
Diamond na DVoice
Image: Instagram

Mkurungezi mkuu na mwanzilishi wa Lebo ya Wasafi Diamond Platnumz alikuwa ni mwenye furaha baada ya kumtambulisha msanii mpya ili kushirikiana nao kusukuma gurudumu la muziki wa Bongo kwenye Lebo la Wasafi.

Msanii huyo 'D,Voice' alitambulishwa rasmi na Bosi wake kupitia hafla ya kufana 'Swahili Night' iliyoandaliwa ili kumkaribisha .

D VOICE  ambaye ndiye atakayekuwa  msanii mchanga sana kwenye Lebo la Wasafi atajumuika na wasanii wengine kwenye Lebo hiyo akiwemo Msanii Zuchu, Mbosso na Msanii Lavalava ambao wote wako chini ya Bosi wao Diamond.

Diamond kwenye hafla hiyo alisimulia kuwa nia yake kwa Kumtabulisha D VOICE ni kumlea kama mwanamuziki na kuchipua nyota yake kwani ni mwanamuziki mchanga mwenye bidii na heshima.

Kwenye mahojiano ya moja kwa moja msanii huyo mpya wa Lebo la Wasafi alisimulia furaha yake huku  akimtaja Diamond  kuwa baba mlezi wa nyota nyingi za wanamuziki wanaochipuka.

"Nilipopata ujumbe kuwa Diamond Platinumz alikuwa na nia ya kunijumuisha kati ya wasanii wa Lebo ya Wasafi kwa kweli nilichanganyikiwa huku machozi yakinitoka kwani sikuwahi fikiria jambo kama hilo...Diamond nilikuwa namuona tu kwa Runinga ilikuwa vigumu kwangu kumfikia ila Mungu ni mwema, Hatimaye ndoto yangu ya muziki itang'aa mikononi mwake," alisema D VOICE.