Kwa mara ya kwanza Diamond ampongeza Harmonize baada ya kushinda Tuzo tatu Marekani

Nashabikia Tuzo za Harmonize kwani nilimlea kimuziki, Diamond alisema

Muhtasari

•Harmonize alishinda tuzo 3 kwa kuwabwaga wasanii wakubwa wa Afrika katika tuzo za African Entertainment Awards

Harmonize na Diamond
Harmonize na Diamond
Image: Instagram

Staa wa Bongo Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza amempongeza msanii Harmonize kwa Tuzo tatu  alizopata Marekani siku chache zilizopita akimtaja kuwa mwanaye aliyemlea kwenye taaluma ya  muziki.

Licha ya kuwa msanii Harmonize alitoka kwenye Lebo la Wasafi kulingana na aliyekuwa bosi wake  Diamond ni furaha kuona vipawa alivyokuza kwa Lebo yake ya Wasafi kuona wakifanikiwa muzikini hadi kutuzwa tuzo kama wasanii  bora.

"Ni furaha kubwa kuona vipawa nizochipua ziking'aa hadi mataifa ya nje, msanii Harmonize kushinda tuzo tatu mfululizo ni furaha kubwa kwetu licha ya kuwa aliondoka wasafi tunafurahi kwa mafanikio yake, kwangu najivunia kwani alikuwa mwanangu niliyemlea kimuziki,"alisema Diamond.

Diamond alisema hayo kwenye mahojiano wakati wa kutambulisha msanii mpya kwenye Lebo la Wasafi huku akisema kuwa ni ndoto yake kuchipua vipawa ili kuwezesha sanaa ya muziki kukua.

Msanii Harmonize alikuwa mmoja wa wasanii chini ya Lebo ya Wasafi ila aliondoka na kuazisha Lebo yake ya 'Konde Music World Wide'.

Harmonize alishinda tuzo 3 kwa kuwabwaga wasanii wakubwa wa Afrika katika tuzo za African Entertainment Awards.

Tuzo ya kwanza aliyoshinda kwa kura nyingi ni tuzo ya msanii bora wa mwaka barani Afrika, akashinda pia video bora ya mwaka kupitia ngoma yake ya Single Again na pia akatajwa kama mfalme wa muziki wa Afrika Mashariki na Bongo Fleva kwa jumla.