Akothee kulipia gauni Sh500 kila siku mwezi mzima baada ya kuhafili 'Pesa sio shida'

“Auu siamini nilifanya. Hii gauni nikichukua. Nitarudisha tarehe 22 Januari hiyo 500 kwa siku sio ishu," Akothee alisema.

Muhtasari

• Akothee kwa furaha alisema kwamba amepitia safari ndefu sana ya kuipata digirii yake ya kwanza na kwa hivyo hatokuwa na haraka ya kurudisha gauni hiyo.

Akothee
Akothee
Image: Instagram

Msanii na mjasiriamali Esther Akoth maarufu kama Akothee ameonesha furaha yake baada ya kujinyakulia kigezo kingine cha kumwezesha kusimama mbele za watu na kupewa heshima.

Akothee ambaye kwa muda sasa amekuwa akiwataarifu wafuasi wake kuhusu maendeleo ya masomo yake ya digrii ya kwanza katika chuo cha Mount Kenya hatimaye amefichua kwamba atahafili mwezi ujao Desemba.

Katika notisi ambayo alipakia kutoka kwa chuo hicho, Akothee na wenzake ambao wanatarajiwa kufuzu walitakiwa kuchukua gauni za kuhafili na kuzirudisha kabla ya Desemba 22, la sivyo watalazimika kuilipia gauni shilingi 500 kwa kila siku baada ya siku rasmi ya kurudisha.

Akothee kwa furaha alisema kwamba amepitia safari ndefu sana ya kuipata digirii yake ya kwanza na kwa hivyo hatokuwa na haraka ya kurudisha gauni hiyo.

Alisema kwamab yeye yuko radhi kukaa nayo hata Zaidi ya mwezi mmoja kutoka siku rasmi ya mwisho ya kurudishwa kwa gauni, akifichua kwamba haoni tatizo katika kulipia shilingi 500 kila siku hadi Janauri 22.

“Auu siamini nilifanya. Hii gauni nikichukua. Nitarudisha tarehe 22 Januari hiyo 500 kwa siku sio ishu 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Siwezi kusubiri siku yangu kuu haki” Akothee alisema.

Mwezi mmoja uliopita, msanii huyo alifichua kwamba alikuwa anatathmini kumualika msanii Beyonce katika sherehe ya tafrija ya baada ya kuhafili.

“Hatimaye nitahitimu Desemba baada ya miaka 14 ya mapambano ya kukamilisha shahada yangu ya usimamizi wa Biashara. Je, umealikwa? Nitag msanii unayempenda niwe naye kwenye mstari wa burudani. Ninafikiria kumualika Beyonce. Hii ni kubwa,” alisema.

Akothee alifichua kwamba atafuzu kutoka chuo kikuu cha Mt Kenya na akasema kwamba alichagua kozi ya HR ambayo imempitisha katika safari ndefu kutoka miji mbali mbali ya Kenya.

 

“Nimebobea katika matumizi wa rasilimali watu katika Chuo Kikuu cha Kenya, kutoka Nairobi hadi Mombasa hadi Kisii 🤣🤣 waaa imekuwa kweli,” alisema akionesha furaha yake.