•Bena amejitetea kwenye mitandao ya kijamii baada ya madai kuwa ameshindwa kuwa mwanaume anayewajibika.
• "Watu wengine watapata njia zote za kukuangusha, wengine wanakushtaki kwa uwongo, wengine watashindwa kukuthamini,"
Bena wa Malines, mtayarishaji wa maudhui mashuhuri wa Kenya amejitetea kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii baada ya madai kuwa ameshindwa kuwa mwanaume anayewajibika.
Mwanadada aliyejitambulisha kama Lydia Waithera alishiriki kwenye mahojiano na wanablogu kwamba Bena amemtelekeza yeye na watoto wake wawili, mmoja ambaye ana umri wa miezi mitatu.
Katika mahojiano hayo alidai kuwa awali Bena alikuwa mtu ambaye anawajibika, na alimshirikisha kabla hajapata umaarufu.
"Alipata umaarufu, akabadilika," alilalamika.
Alisema kwamba mtumbuizji huyo hapatii familia yake kipaumbele kama siku za hapo awali.
Bana huyo hata hivyo amekanusha madai hayo akiwaonya mashabiki wake kutoamini kile wanachoambiwa na kikisikia mitandaoni.
"Mtandao umejaa habari, ukweli fulani, mwingine uwongo, zingine ni za kweli, zingine zimeandikwa. Baadhi yetu tuko hapa kuunda na kuburudisha, na wengine tuko hapa ili kutafuta umaarufu na kukashifu. Usiamini kila kitu ambacho vyombo vya habari hukupa,” mtayarishaji wa maudhui alisema.
Pia alisema siku zote watu watataka kufanya kila wawezalo kuwaangusha wengine licha ya kazi ngumu waliyoifanya ili kufika hapo walipo.
"Watu wengine watapata njia zote za kukuangusha, wengine wanakushtaki kwa uwongo, wengine watashindwa kukuthamini," alisema.
Alionyesha ujumbe wa mama mtoto wake kama njia ya kumchora hasi na kuwahakikishia mashabiki wake kwamba kila kitu kilikuwa sawa na kwamba hakuna chochote cha kuwa na wasiwasi kuhusu.
“Landa ni sapii nguys!” alikiri.
Bena wa Malines alipata umaarufu mwaka wa 2022 wakati mojawapo ya video zake za kuchekesha ziliposambaa mitandaoni. Alisema hiyo ilikuwa video yake ya kwanza kwenye akaunti yake rasmi ya Tiktok.
Video zake zimechochewa na majibizano ya kila siku ambayo anafanya kwa njia ya kipekee inayovutia ambayo huwafanya Wakenya wawe wapenzi wa mitandao yake ya kijamii kwa ajili ya kucheka kutokana na ucheshi wake mkubwa.
Alishinda Tuzo ya Pulse Tiktok ya mshawishi bora wa mwaka mnamo Oktoba 15,2022.