Harmonize ni mdogo wangu ingawa nikiangalia muonekano kidogo kama kanizidi - Rayvanny

Nikiangalia muonekano wake ni kama kidogo kiongozi kanizidi lakini sio mbaya - Rayvanny.

Muhtasari

•"Ni mdogo wangu, tunaongea na anatakiwa arudi na tuzo zangu tatu. Kesho ninaweza nikaja uwanja wa ndege kuchukua tuzo au nikaenda Konde Village,” alisema.

Harmonize na Rayvanny
Harmonize na Rayvanny
Image: maktaba

Msanii Rayvanny amevunja kimya baada ya Harmonize kumtaka amfuate pindi atakapotua nchini Tanzania kutokea Marekani kwa ajili ya kumpokeza tuzo zake za AEUSA2023.

 Akizungumza baada ya kupata tuzo nyingine, Rayvanny alisema kwamba hana uhakika ni wapi atamfuata Harmonize ili kuzichukua tuzo zake kati ya kumwahi katika uwanja wa ndege au kumfuata nyumbani kwake Konde Village.

Msanii huyo kwa utani alisema kwamba yeye ni mkubwa kwa Harmonize kiumri lakini akatilia shaka muonekano wake kwamba huenda amanzidi kwa kutokuwa na uhakika na tarehe zake za kuzaliwa.

“Ataniuwa huyu baba, Harmonize ni mdogo wangu kwa sababu ni mdogo kwangu ingawa sina uhakika na tarehe zake kwa sababu nikiangalia muonekano wake ni kama kidogo kiongozi kanizidi lakini sio mbaya. Ni mdogo wangu, tunaongea na anatakiwa arudi na tuzo zangu tatu. Kesho ninaweza nikaja uwanja wa ndege kuchukua tuzo au nikaenda Konde Village,” alisema bosi huyo wa Next Level Music.

 Rayvanny alifurahia tuzo za mwaka huu akifichua kwamba kuna mwaka alifungiwa na BASATA kama mara mbili lakini mwaka huu ametambuliwa kwa tuzo tatu na kusema kwamba ni mwaka ambao ataukumbuka muda wote.

“Nina furahi sana, hii ni kubwa kwa nchi kwa sababuc unajua unaweza ukawa na huo wimbo ambao watu wamerekodi huko kwao, production ya huko kwao lakini hii yangu ni ya Tanzania kwa kila kitu imefanyiwa hapa, hii ni kubwa,” alisema kwa tuzo hiyo.

Rayvanny alimsifia msanii mpya wa WCB Wasafi, Dvoice ambaye amekuja kuchukua nafasi yake mwaka mmoja tangu alipoondoka.

“Dvoice ni kijana wangu nimeongea naye na huwa tunaongea kabla hajatoka, ni msanii anayetia bidii akaze kwani sababu ndio inaanza,” Rayvanny alisema.