Rayvanny aahirisha kuachia EP kwa heshima ya uzinduzi wa albamu ya Harmonize Nov 24

" Kwa hiyo tumebadilisha nafikiri tutakutana tarehe moja na tarehe 24 utaendelea na mambo yako kiongozi, kwa hiyo ndio hivyo,” Rayvanny alisema.

Muhtasari

• Ikumbukwe Harmonize tangu awali alikuwa ameweka wazi kwamba Novemba 24, wikendi ijayo atakuwa anaachia albau yake ya Visit Bongo.

• Wakati huo huo, pia Rayvanny alikuja baadae na kutangaza kwamba Novemba 24 yiyo hiyo pia atakuwa anaachia EP yake ya ngoma tano kwa mpigo.

 

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE, RAYVANNY

Hatimaye wasanii Rayvanny na Harmonize wamekutana, baada ya ugomvi wao miaka michache iliyopita kufuatia kugonganishwa na familia ya Kajala na bintiye Paula.

Rayvanny alifanya ziara ya kushtukiza nyumbani kwa Harmonize kuchukua tuzo yake ya AEUSA 2023 ambayo Harmonize alimchukulia kutoka nchini Marekani.

Baada ya kukutana, wawili hao waliweza kuzungumzia tofauti zao jinsi zilivyokuwa na kilichowafanya kupatana ili kuzika tofauti na kuanza upya kuinua tasnia ya Bongo Fleva kwa mkupuo.

Ikumbukwe Harmonize tangu awali alikuwa ameweka wazi kwamba Novemba 24, wikendi ijayo atakuwa anaachia albau yake ya Visit Bongo.

Wakati huo huo, pia Rayvanny alikuja baadae na kutangaza kwamba Novemba 24 yiyo hiyo pia atakuwa anaachia EP yake ya ngoma tano kwa mpigo.

Hili lilionekana kuenda kinyume na ‘undugu’ waliokuwa wanauhubiri kwa vyombo vya habari.

Na kufuatia mkanganyiko huo, Rayvanny aliweka wazi kwamba amefanya mageuzi katika kuachia EP yake na kusema kwamba sasa ataisukuma siku yake ya kuachia EP hadi Desemba mosi ili kumuachia Harmonize kutaradadi Novemba 24.

“Iko hivi, ilikuwa nitoe EP tarehe 24 lakini kuna baadhi ya mageuzi kwa baadhi ya nyimbo. Kwa hiyo tumebadilisha nafikiri tutakutana tarehe moja na tarehe 24 utaendelea na mambo yako kiongozi, kwa hiyo ndio hivyo,” Rayvanny alisema.

Hata hivyo, Harmonize kwa kujishaua alisema kwamba alikuwa anatamani wote wamenyane hiyo siku ya Novemba 24 lakini pia akamshukuru Rayvanny kwa kusukuma mbele jambo lake.

“Nashukuru sana lakini nilikuwa natamani hii tarehe 24 iwe ni sikukuu. Lakini kama hivo imetokea ni bahati mbaya wimbo mwingine umeongezwa na vitu kama hivyo lakini tuwashukuru sana, tusije tukaongea vitu vingi tukaharibu,” Harmonize alisema.