‘Form ya Krisi ni ushago’ – Njugush

Akzungumzia ukuaji wa kikundi cha Njugush Creative Team Njugush alisema kuwa kikundi hicho kinafanya vizuri katika tasnia ya sanaa

Muhtasari

• Katika mazungunzo na mwandishi wa habari wa mpasho kalondu,Njugush alisema kuwa sherehe za misimu hasa za Krisimasi huwa za kipekee wakati zinasherehekewa vijijini

• “Krismasi kama sio hocha, hiyo sio Krisi,”

Image: INSTAGRAMU

Mcheshi na muunda maudhui Njugush ameweka nia yake ya kukuza utamaduni wa jinsi ya kusherehekea sherehe za misimu.

Katika mazungunzo na mwandishi wa habari wa mpasho kalondu,Njugush alisema kuwa sherehe za misimu hasa za Krisimasi huwa za kipekee wakati zinasherehekewa vijijini kinyume na zile za mjini.

“Krismasi kama sio hocha, hiyo sio Krisi,”alisema Njigush.

Njugush amezungumza haya huku zikiwa zimesalia siki chache ili kusherehekea sherehe za krisimasi.

Akzungumzia ukuaji wa kikundi cha Njugush Creative Team Njugush alisema kuwa  kikundi hicho kinafanya vizuri katika tasnia ya sanaa na kudhibitisha kuwa mwaka huu kikundi hicho kimeuza vizuri zaidi.

“Huu ndi mwaka ambao tumepanda juu zaidi kulinganisha na hapo awali,”alisema.

Hata hivyo,alisimulia changamoto chache ambazo wanakumbana nazo kama kikundi akisema msimamo dhabiti umewasaidia kuepuka changamoto hizo.

Aliwataka wakenya kuwa imara katika kukabiliana na hali ngumu inayowakumba  huku akiwashauri  kuendelea kuwa na matumaini kwa kila wafanyalo hasa mwaka unapoenda kukalimilika.

“Najua mwaka umekuwa mgumu sana,lakini tunaweza kushinda tukiwa na matumaini bora.Daima tuwe wenye shukrani,” alishauri.

Awali mchesi Njugush alikuwa amezungumzia swala la dhulma ya kijinsia katika famili,huku akieleza mathara yake na jinsi ya kuepuka dhulma hizo.

Katika mazungumzo na wanablogu,Njugush alisema kwamba swala la kudhulumu mtu kijinsia hasa mwanamke limepitwa na wakati na halipaswi kushuhudiwa tena katika jamii.

“Ni lazima watu waache dhuluma za kijinsia, si kwa wanawake tu bali kwa kila mmoja katika familia,ikiwa hamuwezi kutatua maswala ya kifamilia,achana kwa amani,hakuna haja ya kumdhulumu mtu yeyote,kumchapa hakutaleta suluhisho,”alieleza Njigush.