logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Thee Pluto atangaza kufadhili mmoja wa wanafunzi waliofuzu mtihani wa KCPE

Nataka kulipia karo mwanafunzi mmoja kwa shule ya upili Thee Pluto asema

image
na Davis Ojiambo

Burudani24 November 2023 - 06:30

Muhtasari


  • •Mwanablogu huyo amekuwa wa kwanza kujitokeza mitandaoni akiwa na nia ya kumfadhili mwanafunzi yeyote ili kumuwezesha kutimiza ndoto yake
Thee Pluto

Siku moja baada ya matokeo ya mtihani wa darasa la nane KCPE kutangazwa mwanablogu wa mitandao almaarufu Thee Pluto amejitokeza huku akisema kuwa yuko na nia ya kusaidia mmoja kati ya wanafunzi waliofanya mtihani huo.

Muunda maudhui huyo alisema hayo baada ya kushapisha ujumbe kupitia  mtandao wake wa Instagram.

"Natafuta mmoja wa wanafunzi ambao wamefanya vyema kwenye mtihani wa mwaka huu ili kuweza kutimiza ndoto zake ya kujiunga na shule ya upili, lazima awe kati ya wanafunzi ambao wanatoka kwa familia ambaz haziwezi kujikimu kimaisha ,familia ambayo hiwezi kuwa na uwezo wa kusomesha,"alisema Thee Pluto kupitia ujumbe wake kwenye mtandao.

Mwanablogu huyo aliwaomba Wakenya kumsaidia kutafuta mmoja wa wanafunzi hao na kuwasilisha ujumbe kwenye mtandao wake.

"Ikiwa unamfahamu mmoja kati ya wanafunzi ambaye alifanya vyema kwenye mtihani wake naomba muweze kuwasilisha majina yake na matokeo kwenye "DM" yangu alisema.

Mwanablogu huyo amekuwa wa kwanza kujitokeza mitandaoni akiwa na nia ya kumfadhili mwanafunzi yeyote ili kumuwezesha kujiunga na shule ya upili.

Matokeo ya KCPE mwaka huu yamekuwa ya mwisho baada ya kukamilika kwa mtaala wa 8-4-4


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved