logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mchugaji aliyesimamia ndoa ya Akothee na Mr Omosh afunguka

Wanablogu  wanachukulia ndoa ya Akothee kama yao wanachochea -Welly Odendo

image
na Davis Ojiambo

Burudani27 November 2023 - 12:04

Muhtasari


  • • "Cha muhimu ni kuwaombea Akothee na Omosh kwa maisha yao," mchugaji huyu awaambia wanablogu.

Siku chache baada ya wapenzi wawili mwanamuziki Akothee na mpenziwe Omosh kutengana baada ya kuandaa harusi ya kifahari, mhubiri aliyefugisha ndoa hii amefunguka na kusimulia jinsi alizipokea habari hizo.

Mchugaji Welly Odendo kama alivyojitabulisha kwenye mohojiano ya moja kwa moja na wanablogu wa mitandao alisimuli kuwa Kuachana kwa wawili hao kulikuwa kwa hiari yao kwani wao wenyewe ndio walijua masaibu yaliyochangia kuachana kwao.

Hata hivyo mchugaji huyo alisema kuwa kuna haki ya kila mwanandoa kufanya jambo ambalo litaridhisha maisha yake huku akisema kuwa ikiwa ndoa imeshidikana uamuzi wa talaka hutoka kwa wenye ndoa.

"Akothe na Omosh ikiwa walikaa chini wakaona ndoa yao haitafanya kazi hayo ni kulingana na wao wenyewe kwani ndoa ilikuwa juu yao tu hawakufanya kwa ajili ya mtu mwingine," alisema.

Kulingana na mchungaji huyu vyombo vya habari ndivyo vinachukulia jambo hilo kama jambo la kwao ila haliwahusu kwa vyovyote vile kwani ikiwa wawili wameshidwa na ndoa talaka ni kwa manufaa yao.

"Wanahabari wanachukulia ndoa ya Akothee kama yao wanachochea mpaka ikakuwa taarifa kubwa ambayo imekuwa  kauli ya kila siku,"alisema mchugaji huyo.

Kwenye mahojiano hayo na wanablogu mhubiri huyo aliwashauri wambea kuwachana  na ndoa ya Akothee na aliyekuwa Mpenziwe Omosh na kuwatakia mema kwa kuna sababu ambayo ilichangia kusabaratika kwa ndoa yao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved