logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nitakukujia hapo JKIA 'nikufinye' sawasawa KRG amwambia Andrew Kibe

Andrew Kibe,siogopi chochote lazima nisafiri Kenya kwa hafla

image
na

Burudani27 November 2023 - 06:02

Muhtasari


• Hata hivo kwenye mohojiano ya moja kwa moja mwanablogu Andrew Kibe amefunguka wazi na kusema kuwa yeye ahtishiwi na mtu yeyeto na yuko tayari kurejea nchini

Andrew Kibe na KRG

Mwanamuziki almaarufu KRG The Don amemuonya mwanablogu wa mitandao Andrew Kibe kuhusiana na safari yake nchini mwezi ujao akitaja kuwa ni wakati wake mzuri wa kulipiza kisasi  kwa matusi ambayo amekuwa akipokea kutoka kwake

Msanii KRG kwenye Video moja alimkaribisha Mwanablogu Kibe nchini ila kulingana naye kumkaribisha kwake ni kwa kuonana naye uso kwa uso ili kulipiza kisasi.

"Karibu sana najua unapangia kuingia nchini ila nataka kukuahidi  kuwa ahadi ni deni na umefikia wakati mzuri wa kulipa deni yangu nimekuwa tu nikipokea tu matusi na madharau yako kwa muda nami sasa ni wakati wa kulipiza nitakukujia tu wakati utapotua JKIA ili nikufinye sawasawa,"alisema KRG kwenye Video moja.

Hata hivo kwenye mohojina ya moja kwa moja mwanablogu Andrew Kibe amefunguka wazi na kusema kuwa yeye hatishiwi na mtu yeyeto na yuko tayari kurejea nchini kwa hafla moja ambayo itafanyika mwezi wa Disemba.

"Mimi sijatishia mtu yeyote ila mimi husema yale maovu yanafanywa na watu ambayo hayafai kurejea nchini ni lazima sitishwi na jambo lolote nikasafiri na kuhudhuria hafla kama ilivyo mipango yangu alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved