Baraka the Prince aondoka ghafla redioni baada ya Alikiba kutajwa

"Zungumzia muziki wangu, nitakupisha kwenye mahojiano yako kaka,” alisema kwa hasira kabla ya kuondoka.

Muhtasari

• Ghafla, Baraka the Prince alimtishia mtangazaji kwamba angeondoka kabla ya kuondoka kwa shari asitake kusikiliza tena.

Msanii Baraka amemkana Alikiba,
Baraka the Prince, Alikiba Msanii Baraka amemkana Alikiba,
Image: Instagram

Kwa mara nyingine tena msanii Baraka the Prince ameonesha jinsi chuki ilivyokithiri baina yake na bosi wake wa lebo wa zamani, Alikiba.

Msanii huyo alizua kituko katika kituo kimoja cha redio kwa jina Mjini FM nchini Tanzania, baada ya kuondoka kwa fujo studioni mtangazaji alimpotajia jina Alikiba akilenga kumuuliza swali kuhusu rafiki wake wa zamani kwenye lebo ya Kings Music.

Ghafla, Baraka the Prince alimtishia mtangazaji kwamba angeondoka kabla ya kuondoka kwa shari asitake kusikiliza tena.

Msanii huyo kwa dalili zote alionekana kuchefuka roho pindi jina la Alikiba lilipotajwa na akasisitiza kwamba dhamira yake katika stesheni hiyo ni kuzungumzia kuhusu muziki wake wala si kuwataja watu wengine.

“Wewe ongea kuhusu muziki wangu ama nitatoka kwenye mahojiano haya sasa hivi. Zungumza tu kuhusu muziki wangu pekee, sijaja hapa kuzungumzia watu, umetumwa au vipi wewe. Zungumzia muziki wangu, nitakupisha kwenye mahojiano yako kaka,” alisema kwa hasira kabla ya kuondoka.

Itakumbukwa mwaka mmoja uliopita, Baraka the Prince alitangaza wazi kumchukia Alikiba lakini hakuweza kutaja kilichozua nyufa baina yao.

“Ni kweli halafu mimi siwezi kumficha mtu. Kuna vitu vinaitwa vya kibinafsi ambavyo mimi siwezi kuvizungumzia. Ukiishi ukisema kwamba unaezakuwa unawapenda watu wote huo ni unafiki. Kila mtu ana maadui. Kwa hiyo kumchukia mtu sio dhambi na haikatazwi kumchukia mtu,” Baraka the Prince alisisitiza.

 Alijitetea kwa kusema kwamba hata mtoto mdogo anapozaliwa tu tayari ana maadui ambao wanamuona na kumchukia wakati yeye hana tatizo wala laana yoyote. Alisema kwamba Alikiba atasalia kuwa adui wake mkubwa ila akabaki kwenye njia yake kuu kutofichua kiini cha uadui wake na mfalme huyo wa Bongo Fleva.