Harmonize asema majivuno na Chuki vinamaliza muziki wa Afrika mashariki

"Chuki imekita mizizi baina ya wasanii wa Afrika wengi wanaona wamefaulu katika sanaa"

Muhtasari

•Harmonize aliwashauri wasanii  kushikana pamoja ili wamalize chuki ndiposa wafanikishe sanaa ya muziki kwa kuipeleka kwa kiwango cha juu

Harmonize
Harmonize
Image: Insta

Staa wa bongofleva, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amefunguka na kusimulia kuwa muziki wa Afrika mashariki unamalizwa na chuki baina ya wasanii huku akisema kuwa  wengi wao wamejawa  na majivuno.

Msanii huyo aliyasema hayo baada ya  mahojiano ya moja kwa moja na wanahabari wa kituo kimoja cha radio huku akisema kuwa wasanii wa mataifa mengine wanafanikiwa sana kwenye muziki kwa kuwa na umoja kwenye taaluma ya sanaa.

"Chuki imekita mizizi baina ya wasanii wa Afrika wengi wanaona wamefaulu katika sanaa kwa kuwa wana wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo linawafanya kuwa na majivuno,"alisema Harmonize.

Msanii huyo kwenye mahojiano alisimulia zaidi kuwa baadhi ya wasanii wanapendelea miziki yao wenyewe huku akisema kuwa wengi wa wasanii wa Afrika kufanya kolaba ya pamoja imekuwa ni changamoto jambo ambalo wasanii wa mataifa mengine walizika kwenye kaburi la sahau.

"Wasanii wa mengine wameshikana pamoja ndiposa wanapofanya tamasha za miziki kwenye jukwaa kubwa wengi wanajaza kwa kuwa na ukaribu wa pamoja kati ya wasanii na  wafuasi wao,"alisema.

Nyota huyo alitoa mfano wa muziki wa Bongo nchini Tanzania huku akisema kuwa wasanii wakifanya shoo wanataka iwe yao wenyewe mbila ya kujumisha wengi huku akisema kuwa kujipendelea kwingi kwa wasanii ndicho chanzo kikubwa cha muziki wa Afrika mashariki kusosa ladha duniani.

Harmonize aliwashauri wasanii  kushikana pamoja ili wamalize chuki ndiposa wafanikishe sanaa ya muziki kwa kuipeleka kwa kiwango cha juu.