Nyako ameokoa maisha yangu aliyekuwa mtagazaji Kimani mbugua asema

Kimani amesema pesa alizopata zimemuazishia upya maisha

Muhtasari

•Kimani alisimulia kua kwa sasa ana weza kujikimu maisha kwa kuwa na uwezo wa kulipia mahitaji yake

Kimani Mbugua na Nyako
Kimani Mbugua na Nyako

Aliyekuwa mtangazaji, Kimani Mbugua ameeleza jinsi mwanatiktoker maarufu nchini Nyako amebadilisha maisha yake baada ya mchango wa zaidi ya nusu milioni  kupitia wafuasi wake wa mitandao.

"Nyako alibadilisha maisha yangu sikuwa  na mfahamu ila kwa sasa amekuwa mtu wa kupigiwa mfano kwa maisha yangu jinsi alivyojitokeza na kusikia kilio changu aliweza kuwashawishi wafuasi wake kunichangia pesa ambazo kwa sasa nafurahi kwa kuwa nimeanza maisha yangu upya,"alisema.

Kulingana na Kimani Mbugua mwanatiktoker huyo alikuwa  msamaria mwema ambaye alitumwa na muumba wake kumaliza kilio chake na kumuwezesha kupata fahamu ya maisha kwani kwa sasa amepata nyumba ya kukodi na anaweza kumudu mahitaji yake.

Kimani kwa sasa amesimulia kuwa maisha yake yamerudi hali ya kawaida huku akimshukuru Nyako kwa jinsi alijitokeza kuokoa maisha yake.

"Namshukuru sana Nyako kwa mchango wake na ushauri mwema jinsi ambavyo ningetumia pesa hizo kufanikisha ndoto ya maisha yangu tena,"alisema.