Wema Sepetu afunguka mwanamke ambaye hajui kupika hanajishushia heshima

Mwanamke ambaye hajui kuipika ni mzingo kwa jamii-Wema Sepetu

Muhtasari

•Kulingana na Wema kupika ni jambo ambalo wanawake hawawezi kukwepa kwa maana kulingana na mila wanawake ndio wanaofaa kushugulikia upishi

Wema Sepetu
Wema Sepetu

Muigizaji wa vipindi muda mrefu Wema Sepetu amefunguka wazi huku akisema kuwa mwanamke ambaye hajui kupika anajipunguzia heshima  katika familia na hata kwa jamii kwa kuwa wanawake ni viumbe ambao hata kabla wazaliwe kupika huwa kwenye damu.

"Nashagazwa na wanawake wengine ambao wanajivunia kuwa hawajui kupika ilhali kupika ni jambo ambalo liko kwa damu ya wanawake kwa maana kuwa kuna vitu muhimu ambavyo wanawake wanaubwa wakiwa wanavijua ikiwemo kupika mwanamke ambaye hajui kupika ni mzingo mzito kwa familia yake na hata kwa jamii,"alisema Wema Sepetu.

Kulingana na Wema kupika ni jambo ambalo wanawake hawawezi kukwepa kwa maana kulingana na mila wanawake ndio wanaofaa kushugulikia mambo ambayo yanahusiana na vyakula ndani ya familia.

"Kuna baadhi ya wanawake hata kupika yai inakuwa ni changamoto wengine jambo rahisi kama kupika chai inawalea wanawake kama hao kwa kwenye wako na kasoro kwa kuwa jambo hilo ni la aibu ndani ya ndoa,"alisema.

Wema aliyasema hayo huku akimsifia mamake jinsi aliwakanya huku akiwaelekeza kwa njia bora za njisi mwanamke anafaa kuishi na kujifunza mapishi.

"Mamangu kila mara alitukelelesha ikiwa angepata kunatazama Runinga kila mara alitushawishi tuende nyumbani kujifunza mambo ya mapishi,"alisema Wema.