logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanaume hawapendi kuombwa pesa kupima mapenzi yao -Sepetu

Wanaume hawapendi kuombwa pesa kwa kusudi ya kupima mapenzi yao -Wema Sepetu

image
na

Habari30 November 2023 - 06:56

Muhtasari


•Wema alisema kuwa wanawake mwenye tamaa ya pesa wakati ambapo wanaume huwatumia pesa wengi hususia kuwatembelea kwa kuwa hawapedi ushirikiano wa mapenzi baina yao ila kupata pesa zao

Muigizaji wa muda mrefu Wema Sepetu picha Instagram

Muigizaji wa muda mrefu Wema Sepetu amefunguka wazi na kuelezea kuwa wanaume wengi hawapendi tabia za wapenzi wao kuwaomba  pesa  kwa kusudi ya kupima upendo wao kwao.

Kulingana na Wema kumekuwa na tabia nyingi kutoka kwa wanawake kutoamini upendo wa kweli kutoka kwa wapenzi wao jambo ambalo wameiweka kasumba ya kuitisha wanaume wao hela ovyo ovyo ili kutambua iwapo  wanapedwa.

"Wanaume wengi ukerwa na tabia za wanawake kuitisha hela kila mara kwa kusudi la kupima iwapo wanaume wao wanawapenda jambo hili limewafanya wanawake wengi kutoamini mapenzi ya kweli kwa kuleta kasumba ya kutabua uwepo wa mwanaume kwa kumuomba pesa,"alisema Wema.

Wema kwenye ujumbe wake kupitia kituo kimoja cha Radio Wema alisimulia zaidi huku akiwashawishi wanawake kuzigatia upendo wa haki usichochewa na tamaa ya pesa

"Wanawake msije mkajipendekeza kwa wanaume kwa sababu ya pesa zao ikiwa kuna upendo wa kweli kila mwanaume anajua majukumu yake ya kulinda mke wake na familia bila kushawishiwa kutoa pesa,"alisema.

Hata hivyo kwenye mahojina hayo muigizaji wema alitoa kauli huku akisema baadhi ya wanawake mwenye tamaa ya pesa wakati ambapo wanaume huwatumia pesa wengi hususia kuwatembelea kwa kuwa hawapedi ushirikiano wa mapenzi baina yao ila kupata pesa zao.

"Wanaume nawapa ushauri wakati unapokuwa kwenye mahusiano unapotuima mwanamke hela ili akutembelee na kuanza kutoa vijisababu vyoa kutokuja ni wakati mzuri wa kujua kuwa mwanamke yule yuko pale juu ya pesa wala si mapenzi,"alisema.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved