Msanii wa Bongo Fleva azua gumzo kwa kuungama kufanya mapenzi makaburini (video)

“Hatukufanyia kitendo hicho juu ya kaburi la mtu, ilikuwa ni pembeni tu lakini ni ndani kabisa ya makaburi. Tuipomaliza, tuliogopa," alisema.

Muhtasari

• Kayumba alieleza kwamba ulikuwa ni wakati wa usiku ambapo alikuwa anamsindikiza mpenzi wake baada ya kujivinjari naye nyumbani kwake.

Kayumba
Kayumba
Image: Instagram

Kayumba, msanii wa Bongo Fleva kutoka nchini Tanzania amezua maoni kinzani katika mitandao ya kijamii baada ya kukiri waziwazi kwamba aliwahi shiriki tukio la kufanya mapenzi na mrembo wake katika maeneo ya makaburini.

Msanii huyo alikuwa anazungumza kwenye kituo cha Radio cha Furaha FM katika kipindi cha usiku kinachoongozwa na Wema Sepete ambacho maudhui yake haswa yamejikita katika masuala ya mapenzi.

Kayumba alieleza kwamba ulikuwa ni wakati wa usiku ambapo alikuwa anamsindikiza mpenzi wake baada ya kujivinjari naye nyumbani kwake, ghafla walipofika katika maeneo ya makaburini, hisia zikarudi tena na hakuwa na jinsi bali kukata kiu papo hapo.

“Tulikuwa chumbani kwangu, tukamaliza nikatoka kidogo namsindikiza mtoto, tumetoka vizuri kufika katika makaburi hisia zikaamka tena, kama masihara. Mimi binafsi nilishamuomba Mwenyezi Mungu anisamehe lakini sijui mwenzangu kama aliomba. Tulijikuta tunafanya kile kitendo,” alisema.

“Hatukufanyia kitendo hicho juu ya kaburi la mtu, ilikuwa ni pembeni tu lakini ni ndani kabisa ya makaburi. Tuipomaliza, tuliogopa tukasema eeh bwana hapa ni makaburi. Tulikimbizana kabisa,” Kayumba aliongeza.

Ungamo hilo lilivutia maoni kinzani mitandaoni lakini pia hasira kutoka kwa watu ambao wanahisi hiyo ni kukosea marehemu heshima.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya watu kutoka kwa ungamo hilo la kustaajabisha;

“Mimi naogopa hata kupita sembuse kufanya hapana” Marryabass254.

“Duh, dhambi zingine hata Mungu atafikiria mara mbili mbili kabla ya kusamehe, hii yako hatari mzee!” mwingine alisema.

“Kheeeeeeee😂😂😂😂Atakama ndo kuzidiwa loooooo” Officiallilly2020.