Willy Paul ashindwa kuzuia furaha baada ya ngoma yake kutamba Kimataifa

Wimbo huo wa ‘Yes I do’, ambao alimshirikisha mwimbaji wa Jamaika Alaine, unavuma katika nchi mbalimbali kama vile Phillippines na Japan.

Muhtasari

• Kupitia ukurasa wake wa Insta Willi Paul hakusita kueleza furaha aliyonayo kwa jinsi wimbo huo unavyovuma katika mataifa ya kigeni.

• “Mama mwanao amefikia Kiwango cha Kimataifa, Mungu amefanya tena, #I do ndio mwenendo mpya kwenye TikTok. tazama video hizi na ujiunge na mashabiki wangu wa Kimataifa!

Willy Paul
Willy Paul
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki Willy Paul yuko katika shangwe kwani wimbo aliofanya mwaka wa 2017 unavuma sana katika ulingo wa kimataifa.

Wimbo huo wa ‘Yes I do’, ambao alimshirikisha mwimbaji wa Jamaika Alaine, unavuma  katika nchi mbalimbali kama  vile Phillippines na Japan.

Watu wa mataifa hayo sasa wamevuma sana katika mtandao wa TikTok na wimbo wa msanii huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Insta Willy Paul hakusita kueleza furaha aliyonayo kwa jinsi wimbo huo unavyovuma katika mataifa ya kigeni.

“Mama mwanao amefikia Kiwango cha Kimataifa, Mungu amefanya tena, #I do ndio mwenendo mpya kwenye TikTok. tazama video hizi na ujiunge na mashabiki wangu wa Kimataifa! Ni Ngumu Kuamini Lakini ndiyo, rekodi yingine imevunjwa mama! ” alisema katika chapisho hilo.

"Ulimwengu una furaha kwa Willy Paul 😆 🤣 Mkenya, kijana wako anavuma Kimataifa Tena!" aliendelea kusema.

Wimbo huo, uliochapishwa kwenye YouTube mnamo Machi 17, 2017, umepata maoni milioni 37.

Sauti ilitayarishwa na Teddy B huku Samy Dee akiongoza video.

Mashabiki wa Willy Paul wameelezea furaha yao na kupendezwa naye kama ilivyoonyeshwa kwenye maoni.

"Niamini, Willy Paul ni mmoja wa wanamuziki bora tulio nao Kenya.. shida ni moja Kiburi," mtumiaji wa Instagram alisema.

Mwingine aliandika, "unaona Hadi Japanese sidhani kama Kuna msanii mwingine amefika huko."

Wengine pia wamemtaka kuungana tena na msanii wa Jamaika na kuachilia kibao kingine.

Willy Paul na Alaine hata hivyo wana collabo nyingine inayoitwa ‘Shado Mado’. Wimbo huo ulitolewa miaka 4 iliyopita na umepata maoni milioni 3.9 kwenye YouTube.