Ni video ambayo imesambaa na kuenea sana mitandaoni hasa kwenye mtandao wa Tiktok, huku mlezi Mkenya ambaye ameajiriwa Nchini Lebanon akiwaaga watoto wa mwajiri wake.
Sio kuwaaga tu bali video hiyo inaonyesha jinsi watoto hao walijawa na hisia tele wakimuaga mwanamke huyo aliyetambulika kama Rozah.
Baada ya muda mfupi baba mwenye nyumba alionekana akiloa machozi huku watoto wake wakilia pia na kumkimbilia na kumkumbatia Rozah.
Mkurugenzi mtendaji ya Expeditions Maadai Safaris akizungunmzia suala hilo na video hiyo, ameahidi kumtafuta Rozah na kumtunza likizo.
Pia alimpongeza Rozah, kwa ulezi wake bora na kuwa na uhusiano mzuri na watoto wa mwajiri wake, huku ukiashiria kuwa amekuwa mlezi mwema kwa watoto hao.
Ni video ambayo imegusa mioyo ya wengi.
"Kushikwa katika dakika ya mapenzi safi!! Rozah, Mkenya wetu mlezi nchini Lebanon, amegusa mioyo huku video ya TikTok ikionyesha kuaga kwa kihisia kutoka kwa mwajiri wake. Machozi ya watoto yalizungumza mengi kuhusu uhusiano wa kina na wa thamani wanaoshiriki na Rozah. Kama Mkurugenzi Mtendaji wa Expeditions Maasai Safaris, tumeazimia kutambua, kuheshimu na kutuza kujitolea kwa Rozah na kwa kuuonyesha ulimwengu kile ambacho wafanyakazi wa Kenya wanafanywa.
Tafadhali nisaidie kumpata, tungependa kumpa zawadi ya Likizo ya Kukumbukwa ya kulipia gharama zote kama ishara ya shukrani zetu! 🇰🇪
#RewardingRozah #HeartfeltConnections."
Pia kwenye ukurasa wao wa Facebook kampuni hiyo ilisema;
" Bibi huyu wa Kenya mwenye moyo wa Dhahabu anastahili kutambuliwa na kutuzwa kwa kuonyesha ulimwengu kile ambacho wafanyikazi wa Kenya kote ulimwenguni wameundwa - Kujitolea, Shauku na Unyenyekevu. Ona hata watoto hawataki aondoke. Tunataka kumsherehekea na kuwa na likizo ya bure tukimngojea. Tafadhali tusaidie kumpigia/WhatsApp 0783 999 999."