Mkenya anayefanana na Mbosso ataka vipimo vya DNA, adai ni babake aliyemtelekeza

"Haiwezekani kwamba mimi nateseka pahali nje na yeye yuko pale juu yuafaidika na kupata kila kitu na mtoto wake nipo hapa. Yeye yuaona kila kitu macho, pua, maskio na vitendo vyote ni vyake,” alisema kijana huyo.

Muhtasari

• "Yeye yuaona kila kitu macho, pua, maskio na vitendo vyote ni vyake,” alisema kijana huyo.

Mbosso na Demmah B
Mbosso na Demmah B
Image: Facebook

Kwa muda wa miezi kadhaa sasa, kumekuwa na msanii mmoja kutoka chini Kenya ambaye amekuwa akidai kwamba Mbosso ni baba yake.

Msanii huyo chipukizi kwa jina Demmah B ambaye anafanana na Mbosso kwa karibia kila kitu amekuwa akishiriki mahojiano na waandishi wa habari za mitandaoni akisema kwamba hashangai kufanana na msanii wa WCB Wasafi kwani anamfahamu kama baba yake licha ya kuwa hawajawahi kutana hata siku moja.

Msanii huyo sasa amefikia hatua nyingine kwa kudai kwamba anachotaka ni vipimo vya DNA ili kuthibitisha ukweli wake ambao amekuwa akiushikilia kwa muda mrefu.

Demmah B alisema kwamba Mbosso ni baba yake aliyemtelekeza na sasa anateseka huku hali ya kuwa baba yake anapunja maisha mazuri nchini Tanzania.

“Amekataa kabisa, huyo jamaa [Mbosso] tuseme tu ni kama amekataa majukumu, anaogopa DNA. Kwangu mimi niko tayari kufanya DNA tujue kama ni mimi ni mtoto wake, sababu ameniacha nateseka hapa Kenya na babangu yuko kule majuu na ishajua ni yeye, hiyo kitu inaniuma sana,” alisema.

“Yeye yuko tu naona anapost na anajua tu yuko na mtoto hapa Kenya, mtu anakuja tu amepata umetulia anakuapiza kijana unateseka na babaki yuko majuu, inaniumiza sana. Mimi nataka kumuambia Mbosso, chenye nataka kujua ni ukweli tu, tukuje tufanye DNA tujue ukweli uko wapi. Haiwezekani kwamba mimi nateseka pahali nje na yeye yuko pale juu yuafaidika na kupata kila kitu na mtoto wake nipo hapa. Yeye yuaona kila kitu macho, pua, maskio na vitendo vyote ni vyake,” alisema kijana huyo.