Millicent Omanga, Georgina Njenga waongoza orodha ya waliotafutwa zaidi Google 2023

Wawili hao walijipata katika vinywa vya Wakenya kwa siku kadhaa mapema mwaka huu kutokana na kile kilidaiwa kuwa ni video zao za utupu kuvujishwa katika mitandao ya kijamii.

Muhtasari

• Google ilitoa orodha ya watu 10 lakini Wakenya wamechangamkia majina ya wawili hao kwa kashfa ambazo ziliwakumba mwanzoni mwa mwaka huu.

Millicent Omanga na Georgina Njenga.
Millicent Omanga na Georgina Njenga.
Image: Facebook

Huku mwaka ukielekea kutamatika, kampuni ya Google imeachia orodha ya baadhi ya watu na vitu ambavyo Wakenya walitafuta Zaidi katika huduma yao ya utafutaji mtandaoni.

Kwa mujibu wa orodha hiyo katika kipengele cha watu, mwanasiasa Millicent Omanga na aliyekuwa mpenzi wa muigizaji Tyler Mbaya, Georgina Njenga wamejinafasi katika orodha ya watu waliotafutwa Zaidi kwenye Google mwaka wa 2023.

Google ilitoa orodha ya watu 10 lakini Wakenya wamechangamkia majina ya wawili hao kwa kashfa ambazo ziliwakumba mwanzoni mwa mwaka huu.

Majina hayo yalijumuisha Mathe wa Ngara mwanamke anayedaiwa kuwa mlanguzi wa dawa za kulevya huko Ngara, mwinjilisti maarufu wa televisheni Mchungaji Ezekiel, na maafisa wa serikali kama vile Matiang’i, Chebukati, Martha Koome na wanariadha kama vile Faith Kipyegon.

Majina yaliyowavutia zaidi watumiaji wa mtandao ni ya Georgina Njenga, Millicent Omanga na Dj Fatxo.

Omanga alikuwa wa kwanza kwenye orodha huku Dj Fatxo akikamata nafasi ya 3 akifuatiwa kwa karibu na Njenga katika nafasi ya nne.

Omanga ni mwanasiasa mashuhuri wa Kenya, na Fatxo ni DJ wa Mugithi maarufu huku Njenga ni mwanamitindo maarufu wa Instagram aliyejipatia umaarufu baada ya uhusiano wake na Mchezaji nyota ”Baha” kutoka Machachari.

Watu hao watatu walikuwa na kitu sawa kwa kuona kwamba walivuma sana kwa sababu zisizo sahihi.

Mwanasiasa huyo alijipata kwenye jukwaa kuu la umaarufu baada ya video chafu iliyodaiwa kuwa yake, ikimuonyesha akiwa kitandani na kijana mdogo kuachiliwa.

Omanga hajawahi kuzungumzia suala hilo lakini alijibu kwa kuchapisha mstari wa Biblia siku chache baada ya video hiyo kuvuja mapema mwaka huu.

Kesi ya Njenga ilikuwa sawa na ile ya Omanga pekee ambayo yake ilihusisha video za utukutu ambazo zilikusudiwa kuwa gumzo kati yake na mpenzi wake.

Video hizo zilivuja mtandaoni na Njenga akajitokeza kumlaumu mpenzi wake wa zamani aliyekataliwa ambaye inadaiwa hangeweza kustahimili maisha yake mapya yaliyojaa umaarufu na mpenzi mpya.