"Diamond hapendi vitu feki" - Zuchu aitetea cheni ya dhahabu dhidi ya madai ya kuwa feki

Kauli ya Zuchu inakuja miezi kadhaa baada ya Otile Brown kuwaumbua Diamond na Mbosso kuhusu cheni zao walizojitapa nazo kuwa ziliagizwa kutoka nje ya nchi.

Muhtasari

• Diamond amekuwa akishikilia kwamba mikufu na pete zote anazovalia katika mwili wake ni vito halisi.

Diamond na Zuchu.
Diamond na Zuchu.
Image: Instagram

Zuchu amewajia juu baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii ambao wanadai kuwa mikufu ya kifahari ya mpenzi wake Diamond Platnumz ni bandia.

Zuchu alipakia video ya Diamond kwenye Instastory yake akiwa anaonesha mikufu yake ya dhahabu kwenye shingo na kusema kwamba ni halisi kabisa wala hakuna nafasi ya mjadala wa iwapo ni feki au la.

Katika video hiyo, Diamond alikuwa anajitapa kifua kwa kuonesha cheni yake yenye rangi ya dhahabu ambayo ni mfano wa rozali ya kikatoliki yenye msalaba na Zuchu alisema kwamba siku zote mpenzi huyo wake hajawahi kutamani kuvaa kitu chochote ambacho anajua ni bandia.

“Kama si halisi kabisa basi yeye huwa hapendi,” Zuchu aliandika kwenye video hiyo.

Kauli ya Zuchu inakuja miezi kadhaa baada ya Otile Brown kuwaumbua Diamond na Mbosso kuhusu cheni zao walizojitapa nazo kuwa ziliagizwa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuzitumia wakati wa mzunguko wa shoo zao katika tamasha la Wasafi Festival.

Otile alisema kwamba cheni hizo hazikuwa na vito halisi, akiwataka kuwa wakweli kwa mashabiki wao kwani baadhi ya watu kama yeye [Otile] wanajua vito bandia na vito halisi.

Diamond amekuwa akishikilia kwamba mikufu na pete zote anazovalia katika mwili wake ni vito halisi ambavyo aghalau huagizwa kutoka nje ya nchi kwa thamani ghali kusisima haiba yake kuwa msanii nambari moja wa Bongo Fleva Afrika Mashariki.