Harmonize aanza maandalizi ya kuishi na bintiye baada ya tetesi za babymama kuwa mjamzito

Mara kwa mara Harmonize amekuwa akijivunia uzazi wake kwa bintiye Zulekha akijitapa katika mahojiano mbali mbali kwamba yeye sasa ameshakua.

Muhtasari

• “Ninaandaa kitanda chake, acha tuone jinsi kunaonekana,” Harmonize aliandika na kumalizia na emoji za mapenzi za pink vile vile.

Harmonize na bintiye
Harmonize na bintiye
Image: Instagram

Msanii Harmonize ameanza maandalizi ya kumkaribisha bintiye Zulekha Rajab nyumbani kwake Konde Village kwa ajili ya kuishi naye kabisa saa chache tu baada ya tetesi kuibuka kwamba mamake mtoto huyo ambaye walishaachana na Harmonize muda mrefu nyuma, ni mjamzito kwa mwanamume mwingine.

Harmonize alipakia klipu kwenye insta story yake akiwa anaandaa chumba cha kulala chenye mandhari ya rangi ya pink kuanzia kitanda, viti vya mtoto lakini pia midoli.

Msanii huyo kwenye kapsheni alidokeza kwamba anaandaa chumba kwa ajili ya binti yake, kuashiria kwamba hivi karibuni atamhamishia makaazi yake huko Konde Village kutoka kwa mamake, Official Shanteel.

“Ninaandaa kitanda chake, acha tuone jinsi kunaonekana,” Harmonize aliandika na kumalizia na emoji za mapenzi za pink vile vile.

Hatua hii ya Harmonize japo hakuitaja mwenyewe, inaarifiwa ni kutokana na taarifa zilizovujishwa mapema Jumatano kwamba Shanteel, ambaye ni babymama wa Harmonize ni mjamzito miezi michache tu baada ya kuolewa na mwanamume mwingine.

Mara kwa mara Harmonize amekuwa akijivunia uzazi wake kwa bintiye Zulekha akijitapa katika mahojiano mbali mbali kwamba yeye sasa ameshakua.

Katika siku za hivi karibuni, msanii huyo amekuwa akidokeza kumaliza ugomvi na mtu yeyote akisema kwamba kichocheo cha uamuzi huo ni bintiye ambaye hivi karibuni anafikisha miaka 5 na hivyo kuashiria kwamba baba mtu naye ameshakua na anakuza mwana.

Alisema kwamba hatua yake ya kumaliza ugomvi na Rayvanny na hivi karibuni kutarajia kuyamaliza na Diamond ni kumsitiri bintiye katika maisha yake ya ukubwani asije kua akisikia kwamba babake hapatani na mtu Fulani.